VITA KATIKA RASI YA KOREA: KOREA KASKAZINI YAFUNGA MPAKA WAKE NA CHINA



This file photo shows North Korean soldiers patrolling along the bank of the Yalu River in the North Korean town of Sinuiju across from the Chinese city of Dandong.
Picha hii inawaonesha askari wa Korea Kaskazini wakifanya ulinzi kwenye ukingo wa mto Yalu katika mji wa Sijuiju jirani na mji wa China wa Dandong.


Mpaka muhimu kati ya nchi za China na Korea Kaskazini umefungwa dhidi ya watalii kutokana na kuongezea kwa hali ya wasiwasi katika Rasi ya Korea.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na ofisa wa China kwenye Ofisi ya mpaka wa Dandong, kampuni za kitalii haziruhusiwi kupeleka watalii Korea Kaskazini kupitia mpaka huo. Hata hivyo, marufuku hiyo haiwahusu wafanyabiashara.

"Makamuni ya usafirishaji hayaruhusiwi kuwapeleka watalii huko, kwa kuwa serikali ya Korea Kaskazini sasa inawataka wageni waondoke. Kwa kadiri nijuavyo, wafanyabiashara wanaweza kuingia na kuondoka Korea Kaskazini kwa uhuru.”

Hilo linakuja siku moja baada ya Kamati ya Amani ya Eneo la Asia –Pacific nchini Korea Kaskazini kuwashauri wageni wanaoishi huko kuondoka na “kuchukua hatua za tahadhari mapema kwa ajili ya usalama wao.”

Beijing ni mshirika mkubwa wa Pyongyang na kufanya biashara yake kubwa na nchi hiyo kupitia mpaka wa Dandong.

Korea Kusini na Japan zinasema kuwa ziko katika hali ya tahadhari dhidi ya uwezekano wa makombora yanayoweza kurushwa kutoka Korea Kaskazini. Mnamo Aprili 8, Japan pia iliandaa makumbora yake ya kujilinda dhidi ya shambulio lolote kutoka Korea Kaskazini.

Wakati huo huo, Korea Kusini na Marekani zimeongeza harakati zao za kijeshi za pamoja kufuatilia nyendo za Korea Kaskazini na kuiangalia kwa karibu dhidi ya uwezekano wa mashambulizi ya makombora.
Kamanda wa vikosi vya Marekani katika eneo la Pacific, Admirali Samuel Locklear, alisema kuwa Korea Kaskazini imehamisha kiwango kikubwa cha makombora yake ya masafa marefu yajulikanao kama Musudan kwenye pwani yake ya mashariki.

Wasiwasi wa kuzuka kwa vita katika eneo la Rasi ya Korea umeongezeka  kufuatia Marekani kutumia ndege zake aina ya B-52 na B-2 zenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia katika mazoezi ya kijeshi ya pamoja na Korea ya Kusini.

Mnamo Machi 30, Korea Kaskazini ilitangaza kuwa iko katika “hali ya vita” na Korea ya Kusini, ikaonya kuwa uchokozi wowote utakaofanywa na Korea Kusini na Marekani utaibua vita vya Kinyuklia.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment