NDEGE YATUMBUKIA BAHARINI NCHINI INDONESIA


 


Ndege moja yenye abiria wapatao 100 imekosea njia wakati wa kutua na kutumbukia baharini katika kisiwa cha Bali nchini Indonesia.


Msemaji wa shirika la ndege na maafisa wa Serikali wanasema kuwa abiria wote pamoja na wafanyakazi wamepona baada ya ndege ya shirika la ndege la Lion Air aina ya Boeing 737 kukosea njia yake kwenye kisiwa cha Indonesia cha Bali na kutua katika maji ya kina kifupi.

"Ndege hiyo ilikuwa ikitokea Bandung, Java Magharibi, na ilipokaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Bali Ngurah Rai Airport ikashindwa kufikika kwenye barabara ya ndege na kuangukia baharini," anasema msemaji wa shirika la ndege la Lion Air, Edward Sirait.

anasema kuwa kulikuwa na abiria 101 na wafanyakazi saba. Maafisa wanasema kuwa wote walipona lakini hapakuripotiwa majeruhi wowote.

Msemaji wa wizara ya uchukuzi ya nchi hiyo, Bambang Ervan alisema kuwa ndege hiyo iliangukia baharini kabla ya kufika uwanja wa ndege.

Picha za televisheni ziliionesha ndege hiyo ikielea ndani ya maji.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment