MAMIA WAJERUHIWA KATIKA GHASIA NCHINI MISRI



Anti-government protesters throw stones at riot police during clashes in Cairo on March 22, 2013.
Waandamanaji wanaoipinga serikali wakiwatupia mawe polisi wakati wa ghasia zilizozuka mjini Cairo tarehe 22, Machi, 2013.


Watu kadhaa wamejeruhiwa nchini Misri katika ghasia zilizoibuka baina ya wafuasi na wapinzani wa nchi hiyo, Mohamed Morsi.


Ghasia hizo ziliibuka jana katika mji wa Alexandria baada ya swala ya Ijumaa.


Waandamanaji wanaompinga Rais Morsi walikuwa wakifanya maandamano mitaanai ndipo walipokutana na wafuasi wa Rais katika Medani ya Victor Emanuel mjini Alexandria. 

Pande hizo mbili zilishambuliana kwa mawe. Hatimaye vikosi vya usalama viliingilia kati na kutuliza ghasia hizo.

Misri imeshuhudia maandamano ya kuipinga serikali tangu rais Morsi alipoingia madarakani mwezi Juni mwaka jana. Upinzani umekuwa ukitoa madai na tuhuma kwamba anaendesha serikali ya kidikteta.


Mnamo Januari 25, 2011, Wamisri walianzisha mapinduzi dhidi ya Serikali ya zamani ya Husni Mubarak na kuiangusha kabisa mnamo Februari 11, 2011.

Serikali ya Mubarak ilikuwa ikituhumiwa kuwa kibaraka wa Israeli, jambo lililowaghadhabisha raia wengi wa nchi hiyo na kuiangusha katika wimbi la maandamano lililozitikisa nchi kadhaa za Kiarabu.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment