Helikopta moja ya Marekani imeanguka jirani na mpaka wa Korea ya Kaskazini, karibu na kambi ya jeshi ya kaskazini mwa Seoul, vyanzo vya kijeshi vya Korea Kusini na Marekani vimethibitisha.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP lililomnukuu afisa mmoja wa kijeshi wa Marekani, ndege hiyo ya kijeshi ilithibitika kuwa ni helkopta aina ya CH-53. Ilikuwa na wafanyakazi watatu na maafisa wengine 13. Ilianguka wakati wa mazoezi.
Ndege hiyo ilianguka katika eneo la Cheolwon wakati wa mazoezi ya kijeshi ya pamoja kati ya Korea Kusini na Marekani. Mpaka sasa hakuna vifo vilivyoripotiwa kutokana na ajali hiyo.
Uchunguzi unafanyika ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Korea Kaskazini imeyalaani mazoezi hayo ya kijeshi yanayoendelea, ambayo yanafanyika katika kipindi hiki amabcho Korea Kaskazini inajiandaa kujibu mapigo dhidi ya Marekani, Japan na Korea Kusini.
Kuna maoni kuwa Korea ya Kaskazini inaweza kupima uwezo wake wa nyuklia katika kujibu mapigo dhidi ya uchokozi wowote.
Katika kambi hiyo, kuna wanajeshi 28,500 wa kijeshi. Cheolwon limekuwa eneo la matukio mbalimbali: mwaka 1992, askari watatu wa Korea ya Kaskazini wakiwa wamevaa sare za Korea ya Kusini waliuawa, na mwaka 1997, askari watano wa Korea Kaskazini walivuka Eneo Tengefu la mpaka na kuyashambulia maeneo ya Korea Kusini.
CHANZO: RT
0 comments:
Post a Comment