MAREKANI: MLIPUKO WAUA WATU 70 NA MAMIA KUJERHIWA

A smoke cloud rises from an explosion at a fertilizer plant near Waco, Texas, April 18, 2013.
Moshi mzito kutoka katika mlipuko kwenye kiwanda cha mbolea jirani na Waco, Texas, Aprili 18, 2013.



Mamlaka za uokozi katika jimbo la Texas nchini Marekani zinasema kuwa karibu watu 70 wamepoteza maisha na mamia kujeruhiwa katika mlipuko mkubwa uliotokea katika kiwanda kimoja cha mbolea katika jimbo hilo.



Mkurugenzi wa Kampuni ya West Emergency Medical Services (EMS) George Smith amesema kuwa kiasi cha watu 60 mpaka 70 na walifariki na mamia kujeruhiwa leo hii katika mlipuko kwenye kiwanda cha West Fertilizer katika mji wa West, takribani kilometa 32 (maili 20) kaskazini mwa Waco. 

Afisa mmoja katika hospili mjini Waco alisema kuwa aliambiwa atarajie majeruhi 100 kutoka katika eneo la tukio.


Kwa mujibu Naibu Mkuu wa kikosi cha zima moto cha Waco, Don Yeager, kiwanda hicho kilikuwa na vitu mbalimbali vyenye kulipuka, lakini mpaka sasa chanzo hakijulikani.



Vilevile kumekuwepo na taarifa za majengo kadhaa kushika moto, ikiwemo shule.



Sauti za mlipuko huo zilifika umbali wa kilometa 24 (maili 15). 

Kwa mujibu wa kituo cha umeme cha eneo hilo, zaidi ya wateja 2,000 walikosa umeme.



Mnamo Aprili 15, Marekani ilikumbwa na mlipuko mwingine uliotokea katika eneo la mashindano ya mbio za Boston marathon, ukaua watu 3 na kujeruhi zaidi ya 150.



Siku moja baadaye, mamlaka zilikamata barua zenye sumu hatari aina ya ricin, zilizokusudiwa kumfikia Rais Barack Obama na seneta wa Mississippi kutoka chama cha Republican, Roger Wicker. 

CHANZO: Press Tv
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 comments: