
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Benedict XVI anatarajiwa kujiuzulu wadhifa wake kutokana na sabababu mbalimbali zinazohusiana na afya yake. Hayo yamethibitishwa na msemaji wa Vatican.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 85 anatarajiwa kuachia wadhifa wake huo tarehe 28 Februari, baada ya kukanusha habari zilizoenea mwezi Oktoba 2011 kwamba angejiuzulu baada ya kumbukumbu yake ya kufikisha miaka 85.
Benedict, ambaye ni kiongozi wa 265 wa kanisa hilo, alishika nafasi hiyo Aprili 19, 2005.
0 comments:
Post a Comment