![]() |
| VIKOSI VYA MALI |
Mlipuko mkubwa umeutikisa mji wa Gao kaskazini mwa Mali, huku ripoti zikieleza kuwa mapigano yanaendelea baina ya vikosi vinavyoongozwa na Ufaransa na waasi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Aidha, mji wa Gao ulilengwa kwa mashambulizi ya mabomu siku ya Ijumaa na Jumamosi.
Mnao Jumapili, mapigano makali yaliripotiwa katikati ya mji jirani kituo cha polisi, ambapo mwezi uliopita wapiganaji walikitumia kama ngome yao.
Ufaransa ilianzisha vita kwenye nchi hiyo Januari 11 kwa kisingizio cha kuwazuia waasi wasisonge mbele katika mapigano yao. Vita hiyo imewaacha maelfu ya wananchi wa Mali wakiwa hawana makazi.
Mnamo Februari 1, Shirika la Amnesty International lililaani “ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu" uliohusisha mauaji ya watoto katika vita ya Ufaransa nchini Mali.
Shirika hilo la haki za binaadamu lilisema kuwa "kuna ushahidi kwamba kwa uchache raia watano, wakiwemo watoto watatu, waliuawa katika mashambulizi ya ndege" yaliyotekelezwa na vikosi vya Ufaransa dhidi ya Waasi.
Wachambuzi wanaamini kuwa kampeni hiyo ya kijeshi inasukumwa na rasilimali za mafuta, dhahabu na madini ya urani yanayopatikana nchini Mali.

0 comments:
Post a Comment