MWALIMU mstaafu na mwanamke mmoja muuguzi wamefumaniwa wakifanya mapenzi chooni katika baa moja mjini Geita. Mwanaume huyo alikuwa akifundisha katika shule ya msingi Nyamalembo Kata ya Mtakuja wilayani Geita na mwanamke huyo ni muuguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Geita (majina yamehifadhiwa).
Inadaiwa ‘wapenzi’ hao waliamua kufanya kitendo hicho chooni wakihofia kufumaniwa kutokana na ukweli kuwa mwanaume huyo ameoa na mwanamke naye ameolewa.
Kwa mjibu wa mmoja wa wafanyakazi wa baa hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, wawili hao walifika kwenye baa hiyo mchana kupata kinywaji.
Alidai baadaye alishangaa kuwaona wakinyonyana ndimi hadharani hali ambayo ilimfanya awasihi wakatafute sehemu ya kupumzika.
“Nilipowaona wamezidisha kufanya ufedhuli huo niliwasihi kwamba kulingana na taaluma walizonazo watafute sehemu ya kupumzika lakini juhudi zangu hazikuzaa matunda maana hawakukoma,” alisema.
Alidai baadaye aliwaona wakiongozana kuelekea chooni mithili lakini walikawia kurudi na baada ya kufuatilia aligundua tayari wawili hao walikwisha kuanza kufanya mapenzi kwenye choo hicho.
Baadhi ya watu waliozungumza na mwandishi wa habari hizi mbali na kushangazwa na tukio hilo walisema kwa hali hiyo uwezekano wa maambukizi ya Ukimwi kupungua ni mdogo hata kama serikali itatumia mabilioni ya fedha kupambana na maambukizi hayo.
Walisema inasikitisha wanaopaswa kuwa waelimishaji katika janga hilo ndiyo wamekuwa wakiongoza kufanya vitendo vinavyochochea hali hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment