
Polisi wamethibitisha kuwa mji mkuu wa Syria, Damascus umetikiswa na mlipuko mkubwa wa bomu kwenye medani ambayo mikusanyiko ya kuiunga mkono serikali hufanyika.
Polisi wameshindwa kuainisha nini hasa chanzo cha mlipuko huo. Hata hivyo, wameashiria kuwa maafa yaliyotokea yaliwajumuisha pia watoto wanne, kwa mujibu wa shirika la habari za AP.
Wanausalama walieleza pia kuwa mlipuko huo ulitokea kwenye kizuizi cha ukaguzi kilichopo kati ya Ubalozi wa Urusi na makao makuu ya chama tawala cha Rais Bashar Al-Asad cha Baath.
Mwanadiplomasia mmoja wa Urusi alieleza kuwa madirisha ya jengo hilo yalivunjika, lakini hakutoa maelezo zaidi iwapo kuna aliyeuawa au kujeruhiwa katika mlipuko huo.
Vyombo vya habari vya Serikali viliripoti kuwa mlipuko huo ulisababisha maafa, lakini havikuainisha idadi ya watu waliokufa au kujeruhiwa, kwa mujibu wa shirika la habari za Reuters.
Wakati huo huo, mwandishi wa habari wa idhaa ya Kiarabu ya RT alisema kuwa ilitokea milipuko mitatu mjini Damascus, kinyume na ripoti nyingi zinazotolewa sasa hivi.
0 comments:
Post a Comment