HATIMAYE KADINALI O’BRIEN WA UINGEREZA AMEJIUZULU



Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki nchini Uingereza amejiuzulu baada ya kukanusha madai ya “vitendo visivyofaa.”

Siku ya Jumapili Gazeti la Uingereza la Observer liliripoti kuwa makasisi watatu na padre mmoja wa zamani walimshutumu Kadinali Keith O’brien kwa matendo machafu dhidi yao.


O'Brien anasema ameamua kujiuzulu mara moja, siku moja baada ya madai yaliyotolewa na makasisi watatu na padre moja dhidi yake. Hatua hiyo inafuatia madai ya kuwanyanyasa kingono makasisi hao katika miaka ya 1980.  O’BRIEN ndiye kiongozi pekee wa Katoliki kutoka Uingereza anayeweza kupiga kura katika baraza litakalomchagua mrithi wa Papa Benedecto wa 16. O'Brien, mwenye umri wa miaka  74, amekuwa akitetea mapadri na makasisi kuweza kuoa, lakini amekuwa mpinzani mkubwa wa ndoa za jinsia moja. Taarifa zinasema kuwa Papa amekubali hatua yake ya kujiuzulu.

TUTAENDELEA KUWALETEA TAARIFA ZAIDI

CHANZO: Mashirika ya habari

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment