![]() |
| Watoto wa Yemen wakifanyishwa kazi |
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani ILO limetoa ripoti isemayo kuwa zaidi ya watoto milioni 1.3 nchini Yemen wanashirikishwa kwenye ajira za watoto ambapo kati yao takribani nusu milioni wana umri wa kati ya miaka mitano na 11.
Kwa mujibu wa tovuti ya ILO, asilimia 17 ya watoto milioni 7.7 nchini Yemen kati ya miaka 5-17 na asilimia 11 kati ya miaka 5-11 wanashirikishwa kwenye ajira za watoto.
Shirika la Kazi Duniani limetoa wito kwa Yemen kuchukua hatua za kuwalinda watoto na vijana na kufungamana na sheria za kimataifa za kuhakikisha haki zao hazikiukwi. Kwa mujibu wa ILO ajira ya watoto inamaanisha kuwaajiri watoto waliochini ya umri wa miaka 14 jambo ambalo ni kinyume cha sheria za kimataifa na walio kati ya umri wa miaka 14-17 wanaofanya kazi kwa zaidi ya masaa 30 au wanaofanyakazi katika mazingira hatari. ILO inasema zaidi ya watoto milioni 215 wanafanyishwa kazi duniani kote huku zaidi ya nusu yao wakipitia hali ngumu zikiwemo dhuluma za kijinsia na kazi za kulazimishwa.
CHANZO: IRIB

0 comments:
Post a Comment