
Wabunge wa Tanzania wanatazamiwa kupata nyongeza ya posho na marupurupu katika fremu ya marekebisho mapya ambayo yatabadilisha kwa kiasi kikubwa mwenendo wa uendeshaji Bunge.
Duru zinaarifu kuwa iwapo mabadiliko hayo mapya yataidhinishwa, siku za kufanyika mikutano ya Bunge na vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge zitaongezeka.
Kuongezeka kwa posho na marupurupu ya wabunge, maofisa wa Bunge na mawaziri kutazidi kupandisha kipato wanachopata kila mwezi. Wananachi wa Tanzania sawa na wenzao wa Kenya wamekuwa wakilalamika kuwa wabunge na mawaziri wanapata kipato cha juu sana ikilinganishwa na mwananchi wa kawaida. Katibu wa Bunge la Tanzania,
Dk. Thomas Kashilillah amethibitisha kuwepo mjadala kuhusu mabadiliko na kuongeza kuwa iwapo suala hilo litaafikiwa, uamuzi utatangazwa mapema mwezi ujao.
Katika nchi jirani ya Kenya waandamanaji walimiminika barabarani jijini Nairobi siku ya Jumatano kuonyesha hasira zao kwa hatua ya bunge la kumi kupitisha mswada wa kujipatia mabilioni ya pesa kama marupurupu ya kustaafu.
0 comments:
Post a Comment