Wanawake 42 wafikishwa kizimbani kwa kujiuza

WANAWAKE 42 wanaojiuza miili yao wamefikishwa katika Mahakama ya Jiji kujibu mashitaka yanayowakabili. Mwendesha Mashitaka, Richard Mwangori, aliwasomea shitaka lao juzi mbele ya Hakimu Timoth Lyon na kudai watuhumiwa walitenda kosa hilo Januari 15, mwaka huu, saa tano usiku katika eneo la Sinza Vatican.

Kati ya watuhumiwa 42, waliokiri shitaka hilo ni 15 na wengine 27 walikana shitaka hilo.

Kati ya watuhumiwa hao watatu walikuwa na watoto wadogo ambapo wawili wana miezi mitatu na mmoja ana miezi tisa.

Baada ya kuwahoji kwa sababu gani wanafanya biashara hiyo, walijibu wanafanya biashara hiyo kutokana na ugumu wa maisha.

Watuhumiwa waliokiri makosa yao, walipewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miezi sita kwa ajili ya kuwa fundisho katika jamii.

Watuhumiwa watatu wenye watoto wadogo ambao ni Rose John (21), Clara Omary (20) na Ester Salumu (29) walipunguziwa adhabu kutokana na kunyonyesha.

Wanawake hao wenye watoto walipoulizwa wanaume waliozaa nao watoto wako wapi, kila mmoja alisema hana mwanamume.

Hata hivyo, Hakimu Lyon, alisema badala ya kutumikia kifungo cha miezi sita, watatumikia kifungo cha nje kwa muda wa miezi mitatu.

Watuhumiwa waliokana shitaka lao wametakiwa kuwa na wadhamini wawili wakiwa na bondi ya Sh 100,000 kwa kila mmoja pamoja na vitambulisho vinavyowatambulisha kuwa ni wafanyakazi serikalini.

Baadhi ya watuhumiwa hao wapo nje kwa dhamana hadi Januari 29, 2013, kesi yao itakaposomwa tena.

CHANZO: MTANZANIA
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment