![]() |
| Mabaki ya nyumba za marehemu Ernest Mholela zilizobomolewa kabla ya kumzika akiwa hai kutokana na kutuhumiwa kuwa mchawi. |
UPIGAJI ramli na imani za kishirikina vimetajwa kuwa moja ya sababu za watu wawili kuzikwa wakiwa hai na maiti katika tukio lililotokea wiki iliyopita katika Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya.
Ernest Molela anayekadiriwa kuwa na umri zaidi ya miaka 60 na Mizinala Nachela (50), walizikwa hai pamoja na mwili wa aliyekuwa Mkazi wa Kijiji cha Kalungu, Marehemu Nongwa Hussein Januari 13, mwaka huu.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kijijini hapo na maeneo ya Kamsamba na Mkulwe kwenye Kata ya Ivuna kwa takriban wiki moja sasa, umebaini kuwa wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakiamini zaidi tiba ya kienyeji kuliko matibabu ya kitaalamu yanayopatikana hospitalini.
Wakazi hao wamekuwa wakikimbilia kwa waganga wa jadi kutafuta tiba hata ya magonjwa ya malaria, kifua kikuu na homa za matumbo, ambayo yangeweza kutibika kwa urahisi hospitalini.
Mkazi wa Kijiji cha Ivuna, Mark Masepe alitaja magonjwa yanayowasumbua zaidi wakazi wa eneo hilo na kuwafanya wengi wao wakimbilie kwa waganga wa kienyeji kuwa ni malaria na homa ya matumbo.
“Wengi wanaougua magonjwa hayo, wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji, wanaenda kupiga ramli,” alisema mkazi huyo.
Alipoulizwa kwa nini wakazi hao hawataki kwenda hospitalini, alijibu, “Kwanza hospitali zenyewe ni chache, lakini wanaamini kuwa gharama hospitalini ni kubwa kuliko kwa waganga wa kienyeji.”
Ndugu wa marehemu walonga
Mama mzazi wa Marehemu Nongwa Hussein aliyefariki dunia na kuzikwa na waliokuwa hai, Nevelina Kamwendwe (75) alisema mtoto wake ni miongoni mwa wagonjwa waliokuwa wakitibiwa kwa waganga wa kienyeji.
Mama mzazi wa Marehemu Nongwa Hussein aliyefariki dunia na kuzikwa na waliokuwa hai, Nevelina Kamwendwe (75) alisema mtoto wake ni miongoni mwa wagonjwa waliokuwa wakitibiwa kwa waganga wa kienyeji.
Alisema mwanawe alikuwa akiugua ugonjwa usiofahamika katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita. Aliwahi kupelekwa katika Hospitali ya Ifisi iliyoko Mbeya Vijijini ambako alipangiwa upasuaji.
“Mwanangu alikuwa akivimba mwili mzima tulimpeleka hospitalini Ifisi walimpatia dawa ili eti ugonjwa ujikusanye ili waweze kumfanyia operesheni, Lakini hatukurudi tena hospitalini hapo. Tulimpeleka kwa mganga ambako alirudi siku moja kabla ya kufariki dunia,” alisema.
Akizungumzia vurugu zilizosababisha watu wawili kuzikwa hai katika kaburi moja na mwanawe, Kamwendwe alisema, akiwa katika maombolezo wakisubiri muda wa mazishi, lilifika kundi kubwa la vijana likiwa limemshikilia mzee mmoja (Ernest Mholela, kwa sasa ni marehemu) wakimwamuru abebe maiti kupeleka makaburini.
“Baadaye nilimwona Mwajuma Milio (ambaye ni shangazi wa Marehemu Nongwa Huseni) naye amekamatwa na kuanza kuburuzwa,” alisema na kuongeza:
Baada ya Milio kukamatwa, alipelekwa hadi kwenye nyumba yake wakimwamuru atoe dawa anazotumia kuulia watu na baadaye nyumba hiyo kuchomwa moto.
“Baada ya tukio hilo walikwenda moja kwa moja hadi makaburini ambako baada ya kufukia kidogo mwili wa Nongwa, waliwatumbukiza watu hao wote wawili kaburini, kisha kuanza kutupia udongo hadi kujaza kaburi. Walipomaliza walitawanyika,” alisema.
Mtoto mkubwa wa Milio, Flavia Januari alisema kifo cha mama yake kimemsikitisha mno kiasi cha kushindwa cha kuzungumza.
Alipoulizwa kama kulikuwa na mgogoro wowote kati ya familia ya mjomba wake au mama yao, alikanusha akisema, “Hapana kabisa. Siku zote tumekuwa tukiishi kwa uhusiano mzuri.”
Mtoto wa marehemu aliyezikwa hai, Ernest Mholela aitwaye Changala Ernest alisema msiba wa baba yao umewaacha katika simanzi kubwa hasa ikizingatiwa kuwa bado ni wadogo ambao walikuwa wanahitaji matunzo kutoka kwa mzazi huyo.
“Baba amekatishwa maisha, ametuachia pengo kubwa sisi watoto watano ambao wote bado ni wadogo, pia kubomolewa kwa nyumba yetu inatuletea simanzi zaidi maana hatuna pa kwenda hivi sasa,” alisema Changala.
Kauli ya mwenyekiti
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nankanga kulikotokea mauaji hayo, alisema alipokuwa anaingia katika eneo la msiba, alizingirwa na kundi la vijana ambalo lilimteka, kumpiga na kumnyang’anya simu yake ya mkononi.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nankanga kulikotokea mauaji hayo, alisema alipokuwa anaingia katika eneo la msiba, alizingirwa na kundi la vijana ambalo lilimteka, kumpiga na kumnyang’anya simu yake ya mkononi.
“Wakati wote mambo hayo yanafanyika mimi nilikuwa chini ya ulinzi wa vijana hao,” alisema. Aliendelea, “Baada ya kukamilisha unyama wao huo, waliniachia na kuniamuru nirudi nyumbani. Baada ya hapo, simu yangu walinirudishia siku inayofuata.”
Mauaji yalivyofanyika
Awali, Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ivuna, Joseph Silwimba aliliambia gazeti hili kuwa, kabla ya kufukiwa katika kaburi moja na marehemu, watu hao kwa nyakati tofauti walipigwa hadi kuzirai na vijana walioshiriki kuchimba kaburi kwa ajili ya kumzika Hussein.
Awali, Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ivuna, Joseph Silwimba aliliambia gazeti hili kuwa, kabla ya kufukiwa katika kaburi moja na marehemu, watu hao kwa nyakati tofauti walipigwa hadi kuzirai na vijana walioshiriki kuchimba kaburi kwa ajili ya kumzika Hussein.
Silwimba alisema Hussein alifariki Jumamosi saa 10 jioni baada ya kuugua kwa muda mrefu, lakini baadhi ya wakazi wa kijiji hicho walihusisha ugonjwa wake na ushirikina.
Kundi la vijana tisa ambao walikuwa wakichimba kaburi, walianza msako katika Kijiji cha Karungu wakiwatafuta wale waliowatuhumu ni wachawi waliohusika na kifo cha Hussein.
Vijana hao walikwenda nyumbani kwa Mkazi wa Kijiji hicho, George Hussein ambaye ni kaka wa marehemu lakini hakuwapo, hivyo walichoma moto nyumba yake kwa tuhuma za kuhusika na kifo hicho.
“Baada ya kufanya uharibifu huo, walikwenda hadi nyumbani kwa Molela, wakamkamata na kumpiga sana hadi hali yake ikawa mbaya kisha wakambeba hadi eneo la maziko.
“Waliporejea kwenye msiba walimkuta Nachela, naye walimkamata na kumpiga hadi akazimia, ndipo yeye pamoja na Molela waliwatumbukiza kaburini na kuwafukia.
CHANZO: MWANANCHI

0 comments:
Post a Comment