![]() |
| Shimon Peres (kulia) na Yasser Arafat |
Shimon Peres, Rais wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel amekiri kwa mara ya kwanza kuwa utawala huo ulihusika na mauaji ya Yasir Arafat, Rais wa zamani wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina. Peres amesema, Arafat hakupasa kuuliwa kwa sababu ulikuwepo uwezekano wa kufikia maelewano na yeye. Rais wa utawala wa Kizayuni ameongeza kuwa bila ya Yasir Arafat hali ya mambo imekuwa ngumu na tata zaidi.
Mnamo tarehe 12 Oktoba mwaka 2004, Yasir Arafat, alipelekwa Ufaransa kwa matibabu na kulazwa katika hospitali moja ya kijeshi iliyoko kwenye viunga vya mji mkuu wa nchi hiyo Paris. Hata hivyo sio tu hakupata nafuu bali hali yake ilibadilika ghafla na kuwa mbaya zaidi, na mnamo tarehe 11 Novemba mwaka huohuo akafariki dunia hospitalini hapo kutokana na athari ya sumu.
Kwa muda wa miaka miwili kabla ya kufariki kwake, kiongozi huyo wa kwanza wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina alikuwa kwenye kizuizi cha nyumbani alichoekewa na utawala wa Kizayuni huko Ramallah katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Tangu wakati ilipotangazwa habari ya kifo cha Arafat wachambuzi wengi wa mambo, wanaharakati wa kisiasa na hata vyombo vya habari viliamini kuwa kifo chake kilikuwa cha kutatanisha. Ripoti za vyombo vya habari zilieleza kwamba kifo cha Yasir Arafat hakikuwa cha kawaida bali aliuawa kutokana na athari za mada za sumu ya Polonium iliyotiwa kwenye nguo zake. Na tokea wakati huo pia mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya kiongozi huyo ulikuwa ni utawala wa Kizayuni wa Israel ambao kwa muda wote huo haujawahi kukana tuhuma hizo. Kitambo nyuma viongozi wa Palestina pamoja na mke wa hayati Arafat, Suha walitaka maiti yake ifukuliwe na kufanywa uchunguzi tena wa kujua sababu ya kifo chake. Hatimaye mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana maiti ya Yasir Arafat ilifukuliwa na kufanyiwa uchunguzi na wataalamu kutoka nje.
Japokuwa hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi rasmi wa utawala haramu wa Israel kukiri kwamba utawala huo ulihusika na mauaji ya Arafat lakini hata kabla ya kufukuliwa maiti ya kiongozi huyo wa Palestina kwa ajili ya uchunguzi, mkewe, yaani Suha Arafat alikuwa amefichua hapo kabla kwamba Israel ndiyo iliyohusika na mauaji ya mumewe. Hakuna shaka yoyote kuwa kilichomfanya Shimon Peres akiri kuhusika utawala wa Kizayuni na kifo cha Yasir Arafat si matamshi yaliyotolewa na mke wa Arafat bali ni hali mbaya zaidi ambayo imekuwa nayo Israel hivi sasa baada ya kifo cha kiongozi wa zamani wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina.
Kuungama huko kwa Perez kunazidi kudhihirisha sura halisi ya Israel mbele ya fikra za waliowengi duniani. Ukweli wa mambo ni kuwa utambulisho wa Israel una uhusiano na mfungamano wa moja kwa moja na mauaji na ugaidi, isipokuwa kitu pekee kinachoitafautisha Israel na makundi ya kigaidi ni kwamba kundi hilo halina mfungamano wowote wa kiserikali wakati Israel ni dhihirisho halisi la ugaidi wa kiserikali duniani. Nukta nyengine muhimu hapa ni kwamba kukiri kwa Shimon Peres kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel ulihusika na mauaji ya Yasir Arafat kunaweza kuwapa haki ya kisheria viongozi wa Palestina ya kuufungulia mashtaka utawala huo haramu katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai…
CHANZO: IRIB

0 comments:
Post a Comment