Kuna msemo usemao kuwa huwezi kununua penzi. Lakini hali ni tofauti kwa tajiri mmoja wa Kihindi aliyeamua kutumua kiasi cha yuro 14,000 kununua shati la dhahabu halisi ili kuwavutia wanawake.
Tajiri huyo, Datta Phuge, mwenye umri wa miaka 32, kutoka Pimpri-Chinchwad, alitoa kazi hiyo kwa kundi la sonara wapatao 15 ambapo iliwachukua muda wa wiki mbili kuikamilisha kwa wastani wa masaa 16 kwa siku.
![]() |
| MUONEKANO WA DHAHABU: TAJIRI Datta Phuge AMETUMIA ZAIDI YA YURO 14,000 KUTENGENEZA SHATI LA DHAHABU HALISI KUHAKIKISHA ANAWAVUTIA WANAEAKE KWA MASAA YOTE 24 KATIKA ENEO LA KATIKATI MWA INDIA |


Shati hilo lina masijafu yake mawili ya mkononi na seti ya pete zilizochingwa kwa dhahabu.
"Ninajua kuwa mimi sio mwanaume mwenye mvuto zaidi duniani lakini nina hakika kuwa hakuna mwanamke atakayeacha kushangazwa na shati hili" alisema.
"Nimekuwa na ndoto ya kuwa na shati la dhahabu", Bwana Phuge aliliambia gazeti la India la Pune Mirror.
'lItaongeza umaarufu wangu na kujulikana kama 'Bwana Dhahabu kutoka Pimpri"' alisema Bwana Phuge.
Shati hilo lenye urembo liligandishwa kwenye kitambaa cheupe kilichonunuliwa kutoka nje ya India na lina vifungo sita vya Swarovski ya kioo na mkanda wa ndani, vyote vikiwa ni vya dhahabu.
![]() |
| "Ninajua kuwa mimi sio mwanaume mwenye mvuto zaidi duniani lakini nina hakika kuwa hakuna mwanamke atakayeacha kushangazwa na shati hii" alisema. |
CHANZO: DAILYMAIL


0 comments:
Post a Comment