WATU 500 HUUAWA KILA MWAKA KWA IMANI ZA KICHAWI



Imeelezwa kuwa watu wapatao 3000 waliotuhumiwa kuwa ni wachawi, wengi wao wakiwa vikongwe, waliuawa kiholela nchini Tanzania kuanzia mwaka 2005 mpaka 2011. Hayo ni kwa mujibu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC).
“Kati ya mwaka 2005 na 2011, karibu watu wapatao 3,000 waliuawa kiholela na majirani zao waliowadhania kuwa ni wachawi," ilisema ripoti ya kituo hicho.
“Wastani wa watu 500, hususan vikongwe wenye macho mekundu, huuawa kila mwaka nchini Tanzania kwa sababu wanatuhumiwa kuwa ni wachawi," ilibaini ripoti.
Mikoa ambayo vitendo hivyo vimeshamiri ni Mwanza na Shinyanga, imesema LHRC. 
Imani 
“Mkoani Shinyanga, kwa mfano, kati ya Januari 2010 na Januari 2011 pekee watu 242 waliuawa kwa sababu ya watu kuamini uchawi."
Wanawajuaje?
Macho mekundu yanahofiwa kuwa ni alama ya uchawi, hata licha ya ukweli kwamba hali hiyo inaweza kusababishwa na mambo mengine kama vile maradhi na matumizi ya nishati ya kuni katika jamii za vijijini na jamii zenye maendeleo duni.
Inaelezwa kuwa watu wanaamini kuwa uchawi ndio chanzo cha kila tatizo, kuanzia kwenye ugumba, umaskini, kushindwa katika biashara, ukame na hata matetemeko ya ardhi.
Waathirika wengi ni vikongwe ambao wamakumbwa na tatizo la macho kuwa mekundu, tatizo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likichukuliwa kama alama ya kuwa mtu husika ni mchawi.  Watafiti wamegundua kuwa wanawake katika maeneo ya vijijini mara nyingi macho yao hukumbwa na tatizo la macho yao kubadilika na kuwa mekundu kwa sababu ya moshi utokanao na matumizi ya kuni. 
Ramli
Wanawake hao hukumbana na zahma ya kuuawa mara tu mtu fulani anapofariki dunia. Hii ni kwa sababu ndugu wa marehemu huendakwa mpiga ramli kujua sababu ya kifo hicho na mara nyingi huambiwa kuwa kuna mkono wa mtu, au mtu fulani ndiye kamuua kwa uchawi.

Nini Kifanyike?
Inaaminika kuwa elimu na ustawi wa kimaendeleo ni nguzo muhimu sana katika kuzuia na kupambana na mauaji yanayohusishwa na imani za kichawi.

Kimsingi hatuwezi kulitengenishwa suala la uchawi na ukosefu wa maendeleo, ustawi na ustaarabu. Kadiri watu wanavyostawi na kustaarabika ndivyo wanavyoacha kujiingiza katika imani hizo.

Matumizi ya nishati duni, kama kuni, husababisha moshi mwingi ndani ya nyumba, ambao huingia machoni na kuyafanya yawe mekundu.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment