
Hali mbaya ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa na utawala haramu wa Israel imeendelea kuakisiwa kimataifa huku walimwengu wakielezea wasiwasi wao kuhusu kushtadi hatua sisizo za kibinadamu za utawala huo katika eneo hilo. Kuhusiana na hilo Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imetahadharisha juu ya hali mbaya ya sekta ya afya na tiba ya Gaza iliyosababishwa na uhaba wa madawa katika mahospitali na vituo vya afya vya ukanda huo.
Duru za habari za Palestina zimeripoti kuwa, jumuiya ya OIC katika taarifa yake ya Jumamosi juu ya hali ya Gaza ilisema kwamba, zaidi ya madawa 305 kati ya madawa muhimu 478 yamekwisha. Sambamba na kuashiria hali hiyo OIC aidha imesema, suala hilo ni kengele ya hatari inayoashiria kuanza mgogoro wa kibinadamu kwenye eneo hilo la Palestina. Inasemekena kuwa, maisha ya mamia ya wagonjwa wa Kipalestiina huko Gaza yapo hatarini kutokana na ukosefu wa madawa.
Hii ni katika hali ambayo, katika miaka ya hivi karibuni zaidi ya Wapalestina 400 pia wamefariki dunia dunia kutokana na mzingiro wa Gaza. Utawala wa Kizayuni kwa kushirikiana na Marekani kwa karibu miaka 6 sasa unauzingira Ukanda wa Gaza kwa kila upande. Hatua hiyo isiyo ya kibinadamu ya Israel kwa wakaazi wa Gaza ambao pia hushambuliwa kila uchao na utawala huo, imefanya hali ya maisha kwenye eneo hilo kuwa ngumu sana. Pia kuendelea hatua zisizo za kiutu za Israel za kuwazingira Wapalestina zinazokwenda sambamba na hujuma za mara kwa mara za anga, nchi kavu na baharini na mashambulizi ya kiduru dhidi ya Gaza, zimelifanya eneo hilo kukabiliwa na mgogoro mkubwa.
Hatua hizo za Israel zinabainisha kuwa, licha ya kumalizika mashambulizi ya siku 22 ya utawala huo dhidi ya eneo hilo Januari mwaka 2009 na pia vita vya siku 8 vya mwaka huu wa 2012, jinai za Tel Aviv dhidi ya Gaza bado zinaendelea. Kushadidi mzingiro wa Gaza kuanzia mwaka 2007, kivitendo kumewafanya wakaazi milioni moja na nusu wa eneo hilo wakabiliwe na ukosefu mkubwa wa bidhaa na mahitaji ya dharura kama chakula, maji ya kunywa, nguo na dawa na pia kuongeza wasiwasi wa kushtadi mgogoro wa kibinadamu kwenye eneo hilo.
Hatua za kikatili za Israel dhidi ya Wapalestina haziishii tu katika kuwashambulia kinyama, bali utawala huo wa Kizayuni unaendelea kuwaua Wapalestina hasa wa Gaza kwa njia tofauti ukiwemo mzingiro. Kuchelewa jamii ya kimataifa hasa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kali dhidi ya Israel, kumeupa fursa utawala huo uendeleze jinai zake tofauti dhidi ya wananchi wa Wapalestina. Hii ni katika hali ambayo, uungaji mkono wa Marekani na madola ya Ulaya kwa utawala wa Kizayuni unazifanya nchi hizo ziwe washirika wa Israel katika kutekeleza jinai hizo.
CHANZO: IRIB
0 comments:
Post a Comment