Leo, mamlaka za utawala vamizi wa Israeli zimewahamisha watoto wawili kutoka kwenye kijiji cha Kafr Dan magharibi mwa Jenin, na kuwapeleka kwenye mahakama moja ya kijeshi kwa ajili ya kuwashitaki na kuwaunganisha na dazeni za watoto wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za utawala vamizi wa Israeli.
Familia ya watoto hao wawili iliziomba taasisi za haki za binaadamu na vuguvugu la kimataifa la kuwalinda na kuwatetea watoto liingilie kati na kuchiwa huru kwa watoto hao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia hiyo kwa vyombo vya habari, kukamatwa kwa Ihsan Abed (miaka 10) na kaka yake, Ayman Rajeh (miaka 12), ambao walikuwa wameshikiliwa katika gereza la Megiddo, kulifanywa na mamlaka za utawala huo ambao umewahamishia kwenye mahakama ya kijeshi kwa madai na visingizio vya urongo.
Aidha, familia hiyo ilieleza kuwa majeshi ya utawala wa Kizayuni yaliwakamata ndugu hao wawili katika mashamba ya kilimo katika eneo la Marj Ibn Amer siku kadhaa zilizopita na kasha kuwapeleka kusikojulikana.
Kwa upande wake, shirika la kimataifa la utetezi wa watoto lilisema kuwa mamia ya watoto wa Kipalestina, walio chini ya umri wa miaka 18, wanashikiliwa katika jela za Israeli, na wanakumbana na aina mbalimbali za mateso.
CHANZO: Africa to Gaza Aid Convoy
0 comments:
Post a Comment