HOFU YATAWALA KUELEKEA MFUMO WA DIGITALI

Zikiwa zimesailia siku tatu kwa nchi za afrika mashariki kuingia katika mfumo wa matangazo ya digitali kutoka analogia baadhi ya Watanzania wameonyesha kutokuwa tayari na hatua ambazo serikali inachukua kuwezesha mabadiliko ya haraka katika mfumo huo.

Akizungumza katika maojino maalumu juu ya utayari wa mfumo huu Mkurugenzi wa Mawasiliano TCRA Innocent Mongi amesema Mikoa ambayo haijaunganishwa katika masafa ya Digitali haitaathirika na katizo la matangazo ya analogia hapo Desemba 31 mwaka huu.

Kenya inahofiwa kutoingia katika mfumo huu ifikikapo 31/12 baada ya Bodi ya Walaji Nchini humo kuweka pingaimzi wakidai gharama za vingamuzi zipuguzwe kwa mwanachi. 

Desemba 31 inatazamwa na watumiaji wa Televisheni Nchini kama siku yenye kuzua maswali mengi kuliko wajibu wa serikali kuwezesha mabadilko hayo yanayolenga kuihamishia Afrika Mashariki katika mfumo wa Digitali.
Upatikanaji wa Ving’amuzi unatajwa kuwa moja ya vikwazo ambavyo serikali inahitajika kuweka mkakati utakaorahisisha upatikanaji wake kwa watumiaji wote wa vyombo hivyo vya habari.


Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchii wamesema mamlaka hiyo inapaswa kusogeza mbele tarehe ya kubadilisha mfumo wa analogia ili kutowanyiama haki yao ya kupata habari na matangazo mengine muhimu…
Maduka yanayouza Ving’amuzi yamegubikwa na idadi kubwa ya wateja ambao wengi wao hawajawa na elimu ya kutosha kuhusu mabadiliko yanayotarajiwa.


Kwa upande wao TRC wanasema mabadilko haya yatatoa unafuu kwa wakazi wa mikoa ambayo hijaungwa katika masagfa ya Digitali.


Inocent Mongi ni mkurugenzi wa mawasiliano TCRA anasema kuwa hawatazima mitambo ya analojia katika baadhi ya mikoa hiyo kutokana na sehemu hizo kuwa na uhitaji wa kufanya mabadiliko taratibu…


Bodi ya Walaji Nchini Kenya hivi karibuni imeifikisha Mahakamani Tume ya mawasiliano Nchini humo ikiitaka kusogezwa mbele kwa zoezi la kuzima matangazo ya analogia hapo Desemba 31 mwaka huu
Agizo la TCRA linavitaka Vituo vya televisheni kuhamia digitali ifikapo tarehe kama hiyo ambapo kituo chochote kitakachokaidi agizo hilo kitachukuliwa hatua za kisheria .
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment