
Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Tanzania na Malawi kwa pamoja wamekubaliana kwamba Joaquim Chissano Rais Mstaafu wa Msumbiji awe mpatanishi wa mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa. Wakizungumza kwenye kikao cha pamoja na waandishi wa habari mjini Maputo hapo jana, Bernard Kamillius Membe wa Tanzania na Eprahim Mganda Chiume wa Malawi, wamesema kuwa, Chissano ambaye ni Mwenyekiti wa Jopo la Maraisi Wastaafu wa Jumuiya ya Ustawi ya Kusini mwa Afrika SADC ana uwezo wa kuutatua mgogoro huo wa mpaka wa majini baina ya nchi hizo mbili.
Membe na Chiume wamesisitiza kuwa, iwapo Chissano atashindwa kuutatua mgogoro huo, watalazimika kuuwasilisha mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ. Tokea mwezi Agosti mwaka huu, zimeshafanyika duru nne za mazungumzo ya pande mbili juu ya kutatua hitilafu zilizojitokeza za mpaka wa majini wa nchi hizi mbili bila ya natija yoyote.
Mgogoro huo wa zaidi ya miongo mitano umeibuka upya baada ya Malawi kugawa vitalu vya utafutaji mafuta na gesi ndani ya Ziwa Nyasa kwenye eneo la Tanzania.
0 comments:
Post a Comment