Mwanamke mmoja amempiga na kumuua mumewe katika eneo la Barsaloi, Samburu, nchini Kenya baada ya kutofautiana kuhusu mahari ya mabinti zao wawili.
Mwanamke huyo alimuua mumewe, ambaye ni chifu msaidizi, Jumanne usiku.
Mkuu wa polisi ya Samburu kati, OCPD Morris Assila alisema kuwa naibu huyo wa chifu alikuwa amepewa mahari ya mabinti zao wawili lakini hakumpa mkewe fungu lake kulingana na mila na desturi za Wasamburu.
Mgogoro uliibuka na wanandoa hao wakapigana na hapo ndipo mke alipomuua mume.
Assila anasema kuwa mwanamke huyo ametiwa nguvuni na atafikishwa mahakamani.
Mwili wamarehemu umepelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Maralal kwa ajiliya kuhifadhiwa.
CHANZO: STANDARD DIGITAL
0 comments:
Post a Comment