WAZANZIBAR WALALAMIKIA KUUZIWA LAINI ZILIZO SAJILIWA


NA HAMED MAZROUY
 
 
Wananchi  mbali mbali maeneo ya Zanzibar wamekuwa wakilalamikia kitendo cha baadhi ya mawakala wa kampuni za simu za mkononi  kuwauzia line zilizokushasajiliwa kitu ambacho ni tatizo kubwa kwao na kinawapa usumbufu zaidi pale inapotokea line hio kuharinbika au kupotea,wamesema kuwa wanapokwenda kwenye sehemu husika kutaka kurudisha nambari zao wamekuwa wakipata vikwazo vikubwa na kutokufanikiwa kutokana na wahusika hao kutokuweza kuwasaidia tatizo hilo na badala yake wamekuwa wakiwaambia kuwa hawawezi kwani line hio haikusainiwa kwa jina lake halisi.
Kwa upande wao baadhi ya mawakala wanaoshuhulika na uzaji wa line za simu maeneo ya darajani mjini unguja wamesema kuwa wamekuwa wakifanya hivo kutokana na kuepuka usumbufu kutoka kwa baadhi ya wateja wanapofika kununua line wanakuwa hawana vitanmbulisho hivo basi wao hulazimika kutumia majina mengine ili kuweza kusajili line hio pia wamesema wanafanya hivo kutokana na kurahisisha kazi zao.
Aidha mwandishi wa habari hii hakufikia hapa alilazima kumtafuta afisa wa usajili wa line za simu za mkononi kutoka makao makuu ya nzantel daresalam bwana Jorge na amesema kuwa nikweli kuwa baadhi ya wateja wao wamekuwa wakilalamikia kitendo hicho wanachofanyiwa na baadhi ya mawakala wao kitu ambacho sisheria mawakala hao kuwafanyiwa wateja bali walichotakiwa wao ni kuhakikisha kuwa wanasajili line kwa yule wanaemuuzia tu na sio kusajili line kwa jina jengine na kumuuzia mtu mwengine,ameleza kuwa nchi yetu kwa sasa imekabiliwa na wahalifu wengi na wapo baadhi yao ambao hutumuia mitandao kwa ajili yakufanyia kazi zao kutokana na hali hio basi sivyema kwa wakala kumuzia mteja line iliosajiliwa.
Pia ametowa wito kwa wateja wao kuwa wahakikishee kuwa wananunua line zilizosajiliwa kwa majina yao halisi na sio jina la mtu mwengiene,hata hivyo amewataka wateja ambao wataweza kununua line iliosajiliwa kwa bahati mbaya basi afanye mawasiliano kwa kupiga number 106 ili kuweza kubadilishiwa usajili wake wa awali.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment