AJIUA KUTOKANA NA MADENI


Mwanamke mmoja wa Kihispania ameamua kujiua baada ya kushindwa kulipa madeni anayodaiwa na benki ya nchi hiyo. Taarifa zinasema kuwa, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 53 ambaye alichukua mkopo wa nyumba, aliamua kukatisha maisha yake kwa kujirusha kutoka ghorofa ya nne hadi chini. Hatua hiyo ilichukuliwa na mwanamke huyo baada ya mahakama kutoa maamuzi ya kumtaka aondoke yeye na familia yake kwenye nyumba hiyo ya mkopo. Polisi ya Uhispania imeeleza kuwa, hili ni tukio la pili la kujiuwa katika kipindi cha wiki mbili, linalotokana na wateja kushindwa kulipa madeni ya benki. Kwa mujibu wa sheria za Uhispania, mteja akishindwa kulipa deni linalotokana na mkopo wa nyumba, hunyang'anywa nyumba sambamba na kulipa deni lililosalia. Hii ni katika hali ambayo, katika kipindi cha miaka miwili ya hivi karibuni, makumi ya maelfu ya wananchi wa Uhispania wamelazimishwa kuhama kwenye nyumba zao baada ya kushindwa kulipa madeni wanayodaiwa na mabenki ya nchi hiyo.


IRIB
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment