WANAUME WA SAUDI ARABIA HUTUMIWA UJUMBE WA KUWASHTUA KAMA WAKE ZAO WANATOKA NJE YA NCHI



Wanaume wa Saudi Arabia hutumiwa ujumbe kwa njia ya simu kama wake zao watatoke nje ya mipaka ya nchi hiyo. Mfumo huu wa teknolojia umeanzshiswa na serikali ya Saudi Arabia ili kuzuia wanawake wa nchi hiyo wasitoke nje ya nchi bila ruhusa ya waume zao. Mfumo huu umeanza wiki iliyopita baaba ya msafiri mmoja wa kiume akiwa na mke wake kubainisha kuwa alipokea ujumbe unaomfahamisha kuwa mke wake anatoka nje ya mipata ya nchi hiyo wakati wakiwa wote wawili uwanja wa ndege kwa safari ya pamoja. Manal al-Sherif mwanaharakati wa haki za wanawake nchini humo anapinga mfumo huu wa kuwalinda wanawake unaofanya kazi chini ya idara ya uhamiaji nchini humo. 
kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo mwanamke haruhusiwi kuendesha gari. Mwezi wa Juni 2011, wanaharakati wa masuala ya wanawake walianzisha kampeni ya kupinga marufuku hiyo kwa kuamua kuendesha magari yao, huku wengi wakikamatwa na kulazimishwa kusaini wa waraka wa kiapo cha kutoendesha tena.Saudi Arabia ndiyo nchi pekee duniani inayowapiga marufuku wanawake kuendesha gari.
Mwaka jana, Mfalme Abdullah aliwapa wanawake haki ya kupiga kura na kushiriki katika uchaguzi wa miji wa mwaka 2015, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo.

Marufuku nyingi kwa wanawake zimepelekea kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kwa wanawake, kinachokadiriwa kufikia asilimia 30.

 
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment