CHUO KIKUU cha Dodoma, UDOM, kinadaiwa kukumbwa na kashfa ya ngono kufuatia madai kwamba baadhi ya wananafunzi wa kike wanajihusisha na biashara ya kuuza miili yao kwa lengo la kujikimu kimaisha.
Tuhuma hizo zimebainika wakati wa mahafali ya tatu ya UDOM huku takribani wahitimu 6392 wakitunukiwa vyeti,stashahada,shahada za kwanza,uzamili na shahada za uzamivu.
Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho kilianzishwa rasmi mwezi machi mwaka 2007 kimejipatia sifa kemkekm za kitaaluma licha ya ukweli kwamba bado ni kigeni machoni pa wengi.
Tuhuma za ngono miongoni mwa wanafunzi wa kike zinadaiwa kusababishwa na ukata hatua inayowalazimu kutoroka chuoni nyakati za usiku na kujiunga na baadhi ya wasichana wa mitaani waliokubuhu kwenye ukahaba maarufu kama machangudoa kwa lengo la kujiuza.
Wakizungumza na star tv wakati wa mahafali hayo baadhi ya wahitimu wanathibitisha uwepo wa vitendo hivyo vilivyo kinyume na maadili.
Kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof.Idris Kikula anatoa onyo kali kwa wote watakaobainika.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amenukuliwa kwa nyakati tofauti akisisitiza suala la maadili chuoni hapo hatua inayodaiwa kupuuzwa na wanaojihusisha na vitendo hivyo.-Star TV
Tuhuma za ngono miongoni mwa wanafunzi wa kike zinadaiwa kusababishwa na ukata hatua inayowalazimu kutoroka chuoni nyakati za usiku na kujiunga na baadhi ya wasichana wa mitaani waliokubuhu kwenye ukahaba maarufu kama machangudoa kwa lengo la kujiuza.
Wakizungumza na star tv wakati wa mahafali hayo baadhi ya wahitimu wanathibitisha uwepo wa vitendo hivyo vilivyo kinyume na maadili.
Kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof.Idris Kikula anatoa onyo kali kwa wote watakaobainika.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amenukuliwa kwa nyakati tofauti akisisitiza suala la maadili chuoni hapo hatua inayodaiwa kupuuzwa na wanaojihusisha na vitendo hivyo.
About mahamoud
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment