WAKIRISTO WASEMA HAWARIDHISHWI NA RIPOTI YA SERIKALI KUHUSU KUCHOMWA MAKANISA


NA HAMED MAZROUY

Umoja wa Wachungaji wa Makanisa ya Mkoa wa Tanga umesema hauridhishwi na taarifa zinazotolewa na serikali pamoja na viongozi wa siasa kuwa wanaohusika na vitendo vya uchomaji wa makanisa ni wahuni na si Waislamu wakati wanazuoni na masheikh wa taasisi za kiislamu wanakiri kuwa vitendo hivyo vinafanywa na baadhi ya waumini wenzao.

Pia Umoja huo umesema kuwa unashangazwa na kitendo Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi ambaye naye amethibitisha vitendo hivyo kufanywa na makundi ya wahini.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Daresalam jana, Mwenyekiti wa umoja huo, Dk. Jonathan Mwakimage, amesema kuwa serikali inapaswa kushughulikia kiini cha matatizo yanayopelekea kuwepo kwa vitendo vya uvunjifu wa amani hapa nchini kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaowashawishi vijana kufanya vitendo vya kihalifu amabavo vinahatarisha amani ya nchi.

Aidha amesema kuwa wao kama taasisi ya kikiristo hawajaridhishwa na namna ambayo serikali ya Tanzania imekuwa ikishughulikia wahusika wa vitendo hivyo huku baadhi yao wakiendelea kuwa na kiburi na kujiona kuwa wako juu ya sheria ya nchi hii.

Amesema kuwa kwa sasa kumeibuka kundi la watu ambao wamekuwa wakiwashawishi vijana kufanya vitendo vya kuhujumu vitabu vitakatifu jambo ambalo limekuwa likichukuliwa na serikali kama kitu cha kawaida tu.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment