ADAIWA KUMPIGA RISASI MWANAFUNZI MWENZAKE




NA HAMED MAZROUY

Mwanafunzi mmoja wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Kwenjugo wilayani Handeni, mkoa wa Tanga, anaejulikana kwa jina la Nuru Athumani mwenye umri wa miaka (15) ameuwawa kwa kupigwa risasi na mwanafunzi mwenzake.

Mwanafunzi huyo anaedaiwa kuuwawa na mwanafunzi mwenzake anayesoma naye kidato cha kwanza katika shule hiyo kwa kutumia bunduki aina ya Shotgun ambayo ni mali ya baba yake anayedaiwa kuwa ni kigogo wa Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam.

Na kwa upande wao jeshi la polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Coustantine Massawe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea juzi Novemba 11 majira ya saa 4:00 asubuhi katika eneo la Seuta, mjini Handeni.

Na amesema kuwa ni kweli kijana aliyefanya kosa hilo ni mtoto wa mkubwa mwenzetu, kwani unafikiria sisi hatufanyi makosa...hapana, sisi pia ni binadamu kama wengine hivo basi linapotokezea kosa kati nyetu lisichukuliwe vyengine na kuonekana kuwa sisi hatuwezi kutenda kosa

Hata hivyo Kamanda Massawe hakuweza kuelezea kwa undani chanzo cha tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi baada ya kupelekewa taarifa kamili ya tukio hilo kutoka kwa viongozi wa Jeshi la Polisi wa Wilaya ya Handeni.

Aidha kwa Kwa upande wake, mjomba wa marehemu huyo, Rashid Shemweta, alisema marehemu (Nuru) alikwenda na mwenzake kuwinda Kanga katika mtaa wa Seuta wakiwa na bunduki hiyo ndipo mauaji hayo yakatokea.

Amesema kimsingi, mahusiano ya familia hizo ni mazuri na kwamba tukio hilo ni la bahati mbaya tu na bado haijafahamika mara moja kilichotokea hadi kupelekea kutokea kwa mauaji hayo.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment