MGOGORO WA PALESTINA -ISRAELI - GAZA



Mtoto wa Kipalestina aliyejeruhiwa akiwa amelala katika kitanda cha hospitali kufuatia shambulizi la anga la majeshi ya Israeli katika eneo la Beit Lahia, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza leo Novemba 17, 2012. Mashambulizi ya ndege za Israeli yalipiga makao makuu ya baraza la mawaziri wa serikali ya Hamas mjini Gaza, huku mashuhuda wakiripoti kutokea kwa hasara kubwa katika jengo hilo.  AFP





Binti wa Kipalestina akilia wakati wa mazishi ya Audi Naser, aliyeuawa na mashambulizi ya ndege za Israeili. Alizikwa katika eneo la Beit Hanun, kasikazini mwa Ukanda wa Gaza Strip, Novemba 16, 2012.

Ndani ya siku nne, katika Ukanda wa Gaza, Wapalestina 41 wameuawa, wakiwemo watoto 11, na mwanamke mjamzito aliyetegemea kujifungua mapacha. Zaidi ya watu 400 wamejeruhiwa, wengi wao vibaya sana. 

Polisi wa Hamas akilinda jengo la serikali lilioharibiwa na mashambulizi ya ndege za Israeli mjini Gaza.
WATOTO WADOGO WAMEKUWA WAHANGA WA MACHAFUKO NA UKATILI
Kijana wa Kipalestina akiwa amesimama jirani na miili ya Jumana Abu Sefan, mwenye umri wa miezi 18, na kaka yake Tamer, mwenye umri wa miaka mitatu na nusu, wakati wa mazishi yao kwenye msikiti mmoja kasikazini mwa Ukanda wa Gaza leo Novemba 18, 2012. Watoto wote wawili waliuawa katika mashambulizi ya ndege za Israeli yaliyofanywa leo Jumapili, walisema maofisa wa hospitali. Israeli ili iliendelea kuttupa makombora yake kwa siku ya tano mfululizo, huku ikifanya mashambulizi ya angani na majinini na kuliandaa jeshi lake kwa ajili ya uvamizi wa ardhini, japokuwa Misri ilielezea kuwepo kwa "viashiria" vya usitshaji mapigano. 

  Bwana Yoused Abu Khoussa akiwa amebeba mwili mwanaye mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, Iyad, wakati wa ibada ya mazishi kwenye Kambi ya wakimbizi ya Bureij, katikati mwa Ukanda wa Gaza, Leo Jumapili, Nov. 18, 2012.

Mpaka sasa idadi ya Wapalestina waliouawa katika mashambulizi ya Israeli huko Gaza imefikia 74.
 
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment