MGOGORO WA GAZA: TOVUTI YA CHAMA CHA KADIMA CHA ISRAELI YADUKULIWA NA WAPALESTINA


Kiongozi wa Chama cha Israeli cha Kadima, Tzipi Livni

KABUGA KANYEGERI


Tovuti ya chama kikubwa zaidi cha siasa huko Israeli, Kadima, imedukuliwa na Wapalestina wakati utawala huo wa Kizayuni ukiendeleza mashambulizi yake dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Chama cha Kadima, kinachoongozwa na kiongozi wa upinzani, mwanamama Tzipi Livni, kimesema kuwa kiliizima tovuti yake baada ya kuingilwa na wadukuzi (hackers) wa Kipalestina Ijumaa usiku. Blogu ya Livni nayo pia ilidukuliwa.

Taarifa kutoka Israeli zilisema kuwa wadukuzi hao wa Kipalestina pia walizilenga tovuti kadhaa za Israeli ikiwa ni pamoja na tovuti ya Manispaa ya Tel Aviv.

Tovuti ya chama cha Kadima iliwahi kudukuliwa wakati wa Operesheni ya mashambulizi yaliyofanywa na Israeli mwezi wa Desemba mwaka 2008 dhidi ya Ukanda wa Gaza na kuuwa zaidi ya Wapalestina 1,300. 

Hayo yanatokea wakati ambapo Israeli inaendeleza mashambulizi yaliyoanza siku ya Jumatano, dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Kwa uchache Wapalestina 45, wakiwemo watoto wameuawa katika mashambulizi hayo.

Siku ya Jumamosi, wapambanaji wa Kipalestina waliendelea kuilenga miji ya Israeli kwa makombora katika kujibu mashambulizi hayo.

Karibu makombora 650 yameshavurumishwa kwenda Israeli tangu utawala huo wa Kizayuni ulipoanzisha mashambulizi yake.

Makombora ya hivi karibuni kabisa yalirushwa kwenda Tel Aviv Jumamosi asubuhi. Mpaka sasa Waisraeli watatu wamekwishauawa katika mashambulizi hayo.

Ving'ora vimekuwa vikilia katika makazi ya walowezi wa Kizayuni katika mkoa wa Israel wa Nege, pamoja na mji mkubwa kabisa wa Be’er Sheva. Makombora kadhaa yalipiga eneo la wazi katika mji huo Jumamosi asubuhi.

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment