GAZA: JE, KIONGOZI WA QATAR ALIWAUZA HAMAS?



Duru za kuaminika zinasema kuwa, safari iliyofanywa hivi karibuni na Sheikh Hamad bin Khalifa al Thani Amir wa Qatar katika eneo la Ukandawa Gaza, ilifichua makazi ya viongozikadhaa wa ngazi za juu Hamas. Kwa mujibu wa Shirika moja la Habari, Sheikh Hamad bin Khalifa al-Thani aliwapa viongozi wote wa ngazi za juu wa Hamas zawadi za saa za mkononi na kalamu ambazo ndani yake mulikuwa na zana zilizokuwa zikiwasiliana na satalaiti za utawala wa Kizayuni wa Israel na kuwasaidia kuonyesha nyendo zao na mahala wanapoishi viongozi hao.

Ahmad al Ja'abari mmoja kati ya makamanda wa ngazi za juu wa Izzuddin Qassam aliyeuawa shahidi siku chache zilizopita, alilengwa na ndege za kivita za Israel baada ya kufuatiliwa nyendo zake kwa usaidizi wa saa na kalamu alizopewazawadi na Amir wa Qatar. Kwa upande mwengine, imeelezwa kuwa, Amir wa Qatar amemueleza wazi Ismail Haniya Waziri Mkuu wa serikali iliyochaguliwa na wananchi wa Palestina inayoongozwa na Hamas kwamba, kama wanataka misaada ya kifedha kutoka Qatar, wanapaswa kuacha kushirikiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wakati huhuo wautambue rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel.

Aidha Amir wa Qatar alitoa masharti matano kwa Harakati ya Hamas ili iweze kupata misaada ya kifedha na kiuchumi kutoka Qatar, ikiwa ni pamoja na kuacha kushirikiana na Iran, kuanzisha mazungumzo na utawala wa Kizayuni wa Israel bila ya masharti, kuutambua rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel, kuitambua Quds Tukufu kuwa ni mji mkuu wa utawala huo ghasibu na kuacha kabisa muqawama na matumuz ya silaha.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment