BOSI WA CIA AJIUZULU KWA SKENDO YA UZINZI
Mkurugenzi wa CIA David Petraeus amejiuzulu wadhifa wake kutokana na skendo iliyoibuliwa dhidi yake ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa, ambao aliuita kuwa ni "uamuzi dhaifu kabisa." katika barua aliyoituma CIA siku ya Ijumaa,Petraeus alisema kuwa alimuomba Rais Obama akubali ombi lake la kujiuzulu kutokana na matatizo binafsi. "Jana Alasiri, nilienda White House na kumuomba Rais aniruhusu, kwa sababu binafsi, nijiuzulu katika wadhifa wangu kama Mkurugenzi wa CIA.” Petraeus aliandika. "Alasiri hii, Rais alikubaliana na kujiuzulu kwangu." Petraeus, ambaye ametimiza umri wa miaka 60 wiki hii, amekuwa katika ndoa na mkewe Holly kwa miaka 37. Petraeus aliteuliwa kushika nafasi ya Mkurugeni wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) mnamo Septemba mwaka 2011, baada ya kuhuduma kama mkuu wa vikosi vya kigeni nchini Afghanistan vinavyoongozwa na Marekani, akiwa na cheo rasmi cha Kamanda wa Vikosi vya usalama vya Kimataifa ISAF). Obama amemteua naibu wa Petraeus, Michael Morell, kama kaimu Mkurugenzi wa CIA.

0 comments:
Post a Comment