UNESCO: KIWANGO CHA ELIMU TZ NI CHA KUSIKITISHA

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limesema zaidi ya humusi moja (1/5) ya vijana nchini Tanzania hawamalizi elimu ya msingi na hawana ujuzi wa kufanya kazi. Taarifa hiyo imetolewa wakati wa uzinduzi wa 10 wa Mpango wa Kimataifa wa Elimu kwa Wote jijini Dar es Salaam. UNESCO imeeleza kuwa zaidi ya vijana milioni 56 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 walioko Chini ya Jangwa la Sahara hawakumaliza elimu ya msingi wala hawana ujuzi wa kufanya kazi. Pia katika dunia nzima thumni moja (1/8) ya vijana hawana ajira. Kufuatia ripoti hiyo ya UNESCO, Kamishina wa Elimu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya Tanzania, Profesa Eustell Bhalalusesa amesema wizara hiyo inafanya mapitio ya sera ya elimu ili kuhakikisha sekta hiyo inaimarika. IRIB
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment