Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton anasema kuwa ataachia wadhifa wake wakati Rais Barack Obama akijiandaa kwa muhula wa pili wa utawala wake.
Waziri Clinton alitangaza uamuzi wake mapema mwaka huu, akiwaambia wafanyakazi wa wizara ya mambo ya nje kuwa anahitaji kupumzika.
"Bila shaka nitaendelea kuwepo mpaka Rais atakapomteua mtu na mpaka kipindi hicho cha mpito kitakapokamilika, lakini ninadhani kuwa baada ya miaka 20 ya kuwa katika nafasi za juu za siasa za Amerika na changamoto zote nilizokutana nazo, yumkini likawa wazo zuri kugundua ni kwa kiasi gani nimechoka," alisema Clinton.
Tangu Rais alipochaguliwa kwa mara ya pili, msemaji wa Wizara ya mambo ya nje, Victoria Nuland anasema kwamba bado huo ni mpango.
"Mmesikia akisema mara nyingi akisema kuwa anasubiri kumpata mrithi katika kipindi hiki cha mpito na kisha atarejea kwenye maisha binafsi apate kupumzika, kutafakari, kuandika pamoja na mambo mengine," alisema Nuland.
Nani atakayemrithi?
Seneta wa Massachusetts John Kerry ndiye mtu anayetazamiwa sana.
Akiwa kama mwenyekiti wa Kamati ya Seneti ya Mahusiano ya Kigeni, amekuwa mtu muhimu katika sera za nje za Marekani, hasa katika nchi za Pakistan na Afghanistan. Akiwa kama mgombe wa zamani wa urais, ana umaarufu ambao Clinton anautumia katika kuendeleza malengo ya Marekani.
Akiwa kama mwenyekiti wa Kamati ya Seneti ya Mahusiano ya Kigeni, amekuwa mtu muhimu katika sera za nje za Marekani, hasa katika nchi za Pakistan na Afghanistan. Akiwa kama mgombe wa zamani wa urais, ana umaarufu ambao Clinton anautumia katika kuendeleza malengo ya Marekani.
Ndiye mtu ambaye Rais Barack Obama alimteua kusaidia mdahalo dhidi ya mgombea wa Republicna, Mitt Romney, na kampeni ya Obama ilimtumia Kerry katika video ya kumkabili Romney.
"Romney anasema vitu visivyokuwa na ukweli au visivyokubalika na ataka kuziweka hatarini sera zetu za kigeni kwa sababu hafifu za kisiasa," alisema Kerry.
Yumkini kikwazo kwa Kerry ikawa ni kiti chake cha Useneta. Rais anayemchagua seneta kuingia katika baraza lake la mawaziri huwaza iwapo chama tawala kinaweza kukihifadhi kiti hicho. Hususan katika bunge kama la Seneti lenye idadi ndogo ya wabunge.
Juma hili Seneta wa Massachusetts wa chama cha Repuclican Scott Brown alishindwa katika uchaguzi uliokuwa upinzani mkali. Kampeni hiyo iliyokuwa na mchuano mkali inamuweka Brown juu ya wagombea wengine wanaowania kiti kingine cha seneti ya commonwealth kama Kerry atateuliwa kuwa Waziri wa mashauri ya kigeni.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice ni mshindani mwingine muhimu anayeweza kumrithi Clinton.
Akiwa kama mwanadiplomasia katika jiji la New York, yalipo makao makuu ya Umoja wa Matafa, anayemulika yanayotokea katika jukwaa la kimataifa, anaonekana kuwa na nafasi nzuri. Hivyo, kuwa balozi katika Umoja wa Mataifa ni mafunzo makubwa kwa waziri wa mambo ya nje. Alisema mchambuzi mmoja, Madeleine Albright.
Lakini kumteua Rice kunaweza kuibua ukosoaji kutoka kwa maseneta wa Republican kuhusu namna utawala wa Obama ulivyoshughulikia mashambulizi ya mwezi Septemba dhidi ya Ubalozi wa Marekani katika mji wa Benghazi huko Libya yaliyowaua Wamarekani wanne, akiwemo Balozi Chris Stevens.
Hakuna ushahidi unaomhusisha Rice na maamuzi yoyote kuhusu suala la usalama mjini Benghazi. Lakini Rice alikuwa kama sura ya utawala wa Obama siku ya Jumapili kufuatia mashambulizi hayo na alirejea madai kwamba vurugu hizo ziliibuka kutokana na maandamano ya kupinga filamu ya iliyomkashifu Mtume Muhammad (s.a.w). Matukio hayo yamekuwa yakikosolewa vikali.
"Bado kuna maswali memngi ambayo hayajapata majibu kuhusu mashambuli yaliyotokea, na ninadhani hilo linaweza kuwa ndio dhima kubwa kabisa, " alisema mchambuzi wa sera za kigeni katika Taasisi ya Cato, Malou Innocent. "Pamoja na hayo, bado ni mshindani imara katika nafasi hiyo na tutaona kitakachotokea wakati wa kuidhinishwa na bunge la Seneti."
Mtu mwingine anayeonekana katika orodha ya warithi wa Clinton ni Tom Donilon, mshauri wa sasa wa masuala ya usalama wa Taifa wa Marekani. Ni kazi iliyo katika kitovu cha maamuzi ya Rais ya sera za kigeni iliyowahi kufanywa na Henry Kissinger, Colin Powell, na Condoleezza Rice kabla ya kuteuliwa kuwa mawaziri wa mambo ya nje.
Donilon mkongwe aliyehudumu katika utawala wa Bill Clinton, ambapo alihusika sana na upanuzi wa NATO na Makubaliano ya mwaka 1995 ya Dayton yaliyokomesha mapigano katika iliyokuwa Yugoslavia.
"Alihusika sana na sera za Rais Obama za kupambana na ugaidi" alisema mchambuzi kutoka CATO, Malou Innocent. "Vilevile anasikilizwa sana na Rais katika mambo mengi. Lakini, nafikri, anachokosa ni nyota aliyokuwa nayo Waziri Clinton. Hana ushawishi wa kimataifa ambao mtu kama Clinton anao na kitu ambacho unawea kukitarajia katika uhusiano na nchi nyingine."
Hakuna ratiba rasmi ya kuondoka kwa Waziri Clinton. Lakini Rais Obama anaweza kumteua mtu mwingine kabla ya mwisho wa mwaka kwa matarajio ya kumtumia mtu huyo pindi atakapoapishwa kutumikia muhula wa pili wa utawala wake mwezi wa Januari.




0 comments:
Post a Comment