SAYARI YA KWANZA KUWAHI KUWA NA JUA 4
Timu ya kimataifa ya wanaastronomia wametangaza ugunduzi wa sayari ambayo anga zake zinamulikwa na jua nne - ikiwa ni sayari ya kwanza inayojulikana ya aina yake. Sayari hiyo, ambayo iko umbali wa miaka 5000 ya mwanga kutoka Duniani, imepewa jina la PH1 kwa heshima ya watafutaji Sayari (Planet Hunters), mpango unaoongozwa na Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani ambao huwasajili watu wenye kujitolea kuangalia ishara na dalili za sayari mpya. Sayari ya PH1 huzunguka jua 2, huku nayo ikizungukwa na jozi ya pili ya sayari zilizo mbali. Sayari sita pekee ndizo zinazojulikana kuwa zinazizunguka nyota mbili, kwa mujibu wa watafiti, na hakuna yoyote kati ya sayari hizo inayozungukwa na nyota nyingine za mbali. "Sayari za Circumbinary ndiyo sayari maarufu katika muundo wa sayari," alisema Yale wa Meg Schwamb, mwandishi wa Mada iliyowasilishwa siku ya Jumatatu katika mkutano wa kila mwaka wa Idara ya Sayansi ya Sayari ya chama cha wanaastronomia wa Amerika mjini Nevada. "Ugunduzi wa mifumo hii inatulazimisha kurudi kwenye ubao wa kuchorea ili kuelewa jinsi sayari hizo zinavyoweza kukusanyika na kubadilika katika mazingira haya yenye changamoto za mabadiliko." NGUVU YA GESI Wanasayansi, raia wa Marekani na Washirikia wa mpango wa Planet Hunters Kian Jek na Robert Gagliano walikuwa wa kwanza kuitambua sayari ya PH1. Baadaye uchunguzi wao ulithibitishwa na timu ya watafiti wa Uingereza na Marekani wanaofanya kazi zao huko Hawaii. PH1 dude kubwa la gesi yenye kipenyo karibu mara 6.2 ya ardhi, na kuifanya kuwa kubwa kidogo kuliko Neptune. Huzunguka jozi ya nyota zenye kupatwa ambazo ni mara 1.5 na mara 0.41 ya molekuli ya jua takribani kila siku 138. Nyota nyingine mbili zinazunguka mfumo wa sayari kwenye umbali ambao ni takriban mara 1,000 ya umbali uliopo baina ya Dunia na Jua. Tovuti ya Planethunters.org iitengenezwa mwaka 2010 kwa lengo la kuwahamasisha wanaastromia chipukizi kutambua sayari zilizo nje ya mfumo wetu wa jua, kwa kutumia data kutoka katika ya Shirika la Marekani la masuala ya anga NASA Ya Kepler space. Kepler, iliyozinduliwa Machi 2009, ni programu ya kwanza ya Nasa inayoshughulika na utafutaji wa sayari zinazofanana na Dunia ambazo huzizunguka nyota mbalimbali zinazoshabihina na Jua letu. Ugunduzi wa Sayari ya PH1 uliwekwa kwenye tovuti ya arxiv.org siku ya Jumatatu na umewasilishwa kwenye Jarida la Astrofizikia kwa ajili ya kuchapishwa. "Bado inanishangaza jinsi tunavyoweza kubaini, achilia mbali kubariki taarifa nyingi, kuhusu sayari nyingine iliyo kwenye umbali wa maelfu ya masafa ya mwanga kwa kutumia nyota mama" Jek alisema CHANZO CHA HABARI: ALJAZEERA
0 comments:
Post a Comment