RIPOTI: RWANDA NA UGANDA WANAWASAIDIA WAASI WA M23

Jopo la Umoja wa Matafa linasema kuwa waziri wa ulinzi wa Rwanda, anaongoza uasi katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Rwanda na Uganda wanawapa silaha waasi wa kundi la M23. Kundi la wataalamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limesema katika ripoti ya siri kuwa Rwanda na Uganda wameendelea kuliunga mkono Vuguvugu la M23, ambalo linaimarisha udhibiti wake katika majimbo ya Kivu ya Kaskazini na Kivu ya Kusini katika eneo la Mashariki mwa Kongo na linaweza kuhatarisha utawala wa Serikali ya Kongo katika eneo hilo. “Rwanda na Uganda wamekuwa wakiwaunga mkono na kuwasaidia waasi wa M23,” ilisema ripoti hiyo yenye kurasa 44, juzi Jumanne. “Wakati maafisa wa Rwanda wakiratibu uundwaji wa vuguvugu hilo la uasi na pia harakati zake kubwa za kijeshi, msaaada mkubwa wa Uganda kwa kundi la M23 uliliruhusu kundi hilo la Uasi kuwa na tawi la kisiasa likifanya shughuli zake ndani ya Kampala na kuimarisha mahusiano yake na mataifa ya nje", ilisema. “Maafisa wa Rwanda ndio wanaohusika na maagizo ya jumla mipango ya kimkakati ya kundi la M23,” iliongeza ripoti. “Rwanda inaendelea kukiuka vikwazo vya silaha kwa kuwasaidia moja kwa moja waasi wa M23. kuandaa mafunzo, kushawishi na kuwezesha FARDC (Vikosi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) kufanya uasi na utoaji wa silaha na risasi, ushauri wa kiintelelijesnia na kisiasa." “Makamanda wa UPDF (Jeshi la Uganda) walituma vikosi na silaha kwenda kuingezea nguvu operesheni za M23 na kuwasaidia mafunzo na ununuaji wa silaha nchini Uganda," Jopo hilo wa Umoja wa Matiafa lilieleza katika ripoti yake. Uasi huo unaongozwa na Jenerali Bosco Nataganda, ambaye anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC)kwa makosa ya kutoa mafunzo ya kijeshi kwa watoto, na kamanda wa M23, Sultani Makenga ndiye mas-uli wa operesheni na uratibu wa makundi yenye silaha, ilieleza ripoti hiyo ya UM. Ntaganda na Makenga “wote hupokea amri za kijeshi kutoka kwa mkuu wa Majeshi ya RDF (Jeshi la Rwanda), Jenerali Charles Kayonga, ambaye naye hufanyia kazi maagizo kutoka kwa waziri wa ulinzi Jenerali James Kabarebe". Tangu mapema mwezi wa Mei, karibu nusu milioni ya watu wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea mashariki mwa Kongo. Wengi wao wapo ndani ya Kongo, lakini makumi kwa maelfu wamevuka kuingia katika nchi za jirani za Rwanda na Uganda. Waasi wa M23 walijiondoa katika Jeshi la Kongo mwezi wa Aprili kupinga hali mbaya na muamala usioridhisha ndani ya Vikosi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC). Awali, waasi hawa waliingizwa katika jeshi la Kongo chini ya mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2009. Kongo imekuwa ikikabiliwa na matatizo lukuki kwa miongo kadhaa, kama vile umaskini wa kutisha, miundombinu, na vita mashariki mwa nchi, ambavyo kwa zaidi ya muongo mmoja vimewaacha watu milioni 5.5 wakipoteza maisha.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment