UTAFITI: ASILIMIA 40 YA WANAWAKE WANASEMA UONGO KUHUSU HEDHI

Inaelezwa kuwa wanawake hutumia maumivu ya kichwa kama chaguo lao la kwanza kukwepa mahusiano ya kitandani. Utafiti mpya umebaini kuwa, takriban asilimia 40 ya wanawake wamesema uongo kuwa wako katika hedhi ili kutoshiriki tendo la ndoa. Kuanzia kwenye michezo mpaka kwenye mahusiano ya ndoa, ‘kuumwa hedhi’ kunatumika kama kisingizio cha kukwepa kufanya shughuli mbalimbali. Utafiti huo uliofanywa mtandaoni kwa kuwauliza wanawake 1,000 umebaini kuwa asilimia 38 walikiri kuwa huwa wanasingizia hedhi katika mambo mbalimbali. Sababu kubwa iliyotolewa ni kukwepa kufanya mazoezi, huku mwanamke mmoja katika wanawake saba anaitumia hedhi kukwepa tendo la ndoa. Aidha, idadi kubwa – takriban asilimia 20- waliitumia kama kisingizio cha kuwa na tabia ya hasira, kuchukiachukia, usumbufu na kulialia. Wengine husema uongo kuwa wako katika hedhi kama kisingizio cha kutaka kupata muda wa kupumzika. Lakini idadi kubwa hawakujutia kusema uongo- labda kwa sababu karibu nusu ya uongo waliutoa katika simu, ujumbe wa maandishi, mitandao ya kijamii au barua pepe. Utaifiti huo uliofanywa na Panadol, umeeleza kuwa asilimia 90 ya wanawake wanasumbuliwa na tatizo la maumivu yatokanayo na hedhi. Katika asilimia hiyo, asilimia 76 walisema kuwa maumivu yao yalidumu kwa zaidi ya siku moja, ambapo karibu robo ya wanawake wanasumbuliwa na maumivu hayo kwa siku tatu au zaidi. Utafiti uliopita uliashiria kuwa matokeo yake hadi asilimia 10 ya wanawake wanalazimika kuchukua likizo ya kuumwa kila mwezi. Maumivu hayo hunasababishwa na manyweo ndani ya tumbo wakati wa hedhi. Kila moja huacha kutiririsha damu kwa muda na kusababisha tishu zihitajie oksijeni sana. Wakati huo huo, kemikali ziitwazo prostaglandins hutolewa na kusababisha mnyweo mkali na unaweza kusababisha maumivu zaidi. Hali hiyo ambayo pia hujulikana kama dysmenorrhoea, huwafanya baadhi ya wanawake kupata maumivu makali yanayowafanya watapike na kunyong’onyea. Hali hii huwa mbaya zaidi katika umri wa ujana na huendelea kupungua kadiri umri unavyosonga mbele.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment