VIFO VYAONGEZEKA KATIKA MAANDAMANO YA PAKISTAN
Habari zilizopatikana hivi punde zinasema kuwa idadi ya vifo imeongezeka katika maandamano yanayoendelea nchi nzima huko Pakistan.
Maandamano hayo yanafanyika dhidi ya filamu iliyotengenezwa nchini Marekani na vibonzo vya katuni vilivyochapishwa nchini Ufaransa vikimdhalilisha Mtume Muhammad (s.a.w).
Taarifa zilizopatikana hivi sasa zinasema kuwa watu wapatao 19 wamefariki dunia katika maandamano hayo, ambayo ni sehemu ya maandamano makubwa yanayoendelea katika Ulimwengu wa Kiislamu na Afrika.

0 comments:
Post a Comment