KIFO CHA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA, MELES ZENAWI

Image

  • Ndiye Waziri Mkuu wa muda mrefu Afrika Mashariki
  • Amefariki akiwa na umri wa miaka 57
Serikali ya Ethiopia imetangaza rasmi kifo cha Waziri Mkuu wa Muda mrefu zaidi Afrika Mashariki, Meles Zenawi, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 57 baada ya kupambana kwa muda mrefu na maradhi ambayo hayajawekwa wazi.
Kwa mujibu wa tangazo la Serikali lililorushwa na televisheni ya Taifa, Waziri Mkuu huyo alifariki siku ya Jumatatu usiku baada ya ‘kuzidiwa na maradhi.’
Kutokana na kuonesha hali duni ya afya, Waziri Mkuu huyo alilazwa hospitalini mwezi Julai.
Mapema mwezi Agosti, licha ya Waziri Mkuu huyo kutoonekana hadharani kwa takribani miezi miwili mfululizo, msemaji wa Serikali ya Ethiopia alikanuasha taaraifa kwamba alikuwa katika hali tete na akadai kuwa     alikuwa katika “hali nzuri na madhubuti.”
Ripoti zinapendekeza kuwa wakati huo Meles alikuwa akisumbuliwa na tatizo la tumbo kushindwa kufanya kazi na amekuwa akipelekwa katika hospitali moja ya Ubelgiji kwa matibabu makubwa.
Meles, ambaye alishika madaraka muongo mmoja uliopita kama kiongozi wa waasi na kufanikiwa kumuondoa madarakani kiongozi wa wakati huo, Mengistu Haile Mariam, alitawala taifa hilo la Kiafrika kuanzia mwaka 1995 mpaka 2012, na alikuwa mshirika mkubwa wa Marekani katika kile kinachodaiwa kuwa ni vita dhidi ya ugaidi.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment