BOMU LAUA WATU 9 NA KUJERUHI 68 KUSINI –MASHARIKI MWA UTURUKI

Mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari umeua watu 9 na kuwajeruhi wengine 68 katika eneo la katikati ya mji wa kusini-mashariki wa Gazianteb nchini Uturuki.
Mlipuko huo ulitokea jirani na kituo cha Polisi siku ya Jumatatu. Magari kadhaa, ikiwa ni pamoja na gari la mji huo, nayo yaliungua.
Meya wa nji wa Gaziantep, Asim Guezelbey, alithibitisha idadi hiyo ya vifo na majeruhi.
Maafisa wa Uturuki siku zote wamekuwa wamewalaumu wanamgambo wa Chama cha wafanyakazi cha Wakurdi  (PKK) kwa mashambulizi kama hayo.
PKK  ni kikundi cha kigaidi  kilichoanzisha uasi wa silaha na mapambano mnamo mwaka 1984 kwa madhumuni ya kuwa na Dola yao ya Kikurdi kusini –mashariki mwa Uturuki.
Kikiwa kimeorodheshwa na Ankara na jamii kubwa ya kimataifa kama kikundi cha kigaidi, kinashutumiwa na kubebeshwa lawama na Uturuki kwa vifo vya watu 45,000 kwa zaidi ya miongo miwili iliyopita.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment