Kiungo mkongwe wa Misri, Mohamed Aboutrika, amewekwa
kwenye orodha ya ugaidi nchini humo kwa kudaiwa kuunga mkono vuguvugu la Udugu
wa Kiislamu lililopigwa marufuku.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38, ambaye aliwahi
kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji wa mwaka inayotolewa na BBC kwa mwaka 2008 na
ambaye aliichezea timu yake ya taifa michezo zaidi ya 100, anatuhumiwa kuwa
miongoni mwa wafadhili wa chama hicho, ambacho serikali ya Misri inakiona kuwa
ni cha kigaidi.
Aboutrika aliunga mkono waziwazi urais wa Muhammed Morsi
wa chama hicho mwaka 2012. Morsi aliondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo
mwaka mmoja tu baada ya kukalia kiti cha urais.
Mwaka 2015 mali kadhaa za Aboutrika zilishikiliwa na
serikali, na sasa anakabiliwa na hatari ya kunyang’anywa pasipoti yake na
kuzuiliwa kuondoka nchini humo.
Hata hivyo, mwanasheria wake, Mohamed Osman, ameashiria
kuwa uamuzi huo utakatiwa rufaa na kwamba Aboutrika “hajatiwa hatiani au kupewa
taarifa rasmi ya mashitaka yanayomkabili”.
0 comments:
Post a Comment