Timu ya taifa ya Uganda leo watashuka dimbani
kuchuana na timu ya taifa ya Ghana katika uwanja wa Stade Sogara katika mji wa
Port Gentil nchini Gabon ikiwa imepita miaka 39 tangu Uganda iliposhiriki
katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Uganda wamewahi kukutana na Ghana katika mechi tatu
ndani ya miaka mitatu iliyopita. Waghana hawakushinda mechi yoyote dhidi ya
Uganda. Hata hivyo, mtifuano wa leo unatarajiwa kuwa na changamoto kwa Timu
hiyo ya Uganda kutokana na ukweli kwamba Waghana wana uzoefu mkubwa na michuano
hiyo.
“Tangu mwaka 1978, hatujashiriki AFCON mara 19 wakati
Ghana imekuwa ikishiriki michuano hii kila mara. Hivyo, wanakuja uwanjani
wakiwa na uzoefu mkubwa na michuano hii.” Kocha wa Uganda Micho Sredojevic aliambia
Daily Monitor jana mchana kwenye makazi ya timu yake kwenye Hotel Du Parc, ambayo
iko umbali wa dakika tatu kutoka dimba la Stade Sogara
Mlinzi wa timu ya Uganda, Murushid Juuko na Kiungo Khalid
Aucho hawatocheza mecho hiyo ya kwanza kwa sababu wamesimamishwa.
Mkongwe wa soka la Zambia, Kalusha Bwalya, amewaambia Uganda
Cranes wafanye juu chini wasipoteze mechi hii ya kwanza, akisema kuwa timu hiyo
itakabiliana na timu kubwa na kusisitiza kwa kusema ‘ngoja tone namna Uganda watakavyoanza.
Lakini ninawaambieni ni mechi ngumu. Misri, Ghana, Mali, sio timu za mchezo.’
“Mechi ya kwanza katika mashindano yoyote huwa ni mechi
muhimu sana. Tunatakiwa kuingia dimbani kwa nguvu zote kwa sababu timu
tunayopambana nayo ni Ghana. Hatuwazi kuhusu Misri na Mali; mipango na fikra
zetu tunazielekeza kwa Ghana.” Alisema Kocha Micho.
“Tunajua kuwa taifa lote liko nyuma yetu na hii ni fursa
ya kihistoria kwa baadhi yetu ambao tumekuwa katika kikosi hiki kwa muda mrefu.
Hatutaki kuondoka tukiwa na majuto, hivyo kitu pekee cha kufanya ni kutumia
uwezo wetu wote kutimizi matarajio ya Waganda wenzetu.” Alisema kiungo wa Cranes,
Tonny Mawejje
0 comments:
Post a Comment