Bunge la Gambia limepitisha azimio linalomruhusu Rais Yahya
Jammeh kubaki madarakani kwa miezi mitatu zaidi, kuanzia leo, kwa mujibu wa
televisheni ya serikali.
Jammeh, ambaye ameitawala Gambia kwa miaka 22, mwanzo
alikubali kushindwa na Adama Barrow katika uchaguzi w mwezi Desemba, lakini
baadaye aliyapinga matokeo kwa madai kuwa yalikuwa na dosari na kupeleka madai
yake kwenye Mahakama ya Juu ya nchi hiyo.
Barrow anatarajiwa kuapisha Alhamisi.
Mapema Jumanne Rais Jammeh alitangaza hali ya hatari,
siku chache kabla ya muda wa kung’atuka madarakani kuwadia, huku mashirika na
makapuni ya utalii kutoka Uingereza na Ujerumani yakifanya harakati za
kuwaondosha maelfu ya watalii kutoka nchini humo.
0 comments:
Post a Comment