Balozi wa Russia nchini Uturuki aliyeuawa leo mjini Ankara. |
Balozi wa Urusi nchini Uturuki bwana Andrey Karlov,
ameuawa leo Jumatatu kwa kupigwa risasi na mtu mwenye silaha wakati akishiriki
ufunguzi wa maonesho ya picha katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara.
Karlov alizaliwa Februari 4 mwaka 1954 mjini Moscow, na
akahitimu masomo yake mwaka 1976 katika Chuo cha Uhusiano wa Kimataifa cha mjini
humo, ambapo mwaka 1992 alihitimu masomo yake katika Chuo cha Diplomasia
kilicho chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi.
Karlov alianza maisha yake ya kidiplomasia mwaka 1976,
ambapo alishika nafasi mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya Nje ya iliyokuwa
Muungano wa Kisovieti na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Urusi, sambamba na
majukumu mbalimbali ya nje ya nchi aliyokabidhiwa.
Alifanya kazi katika ubalozi wa Muungano wa Usovieti
katika nchi ya Korea Kaskazini mwaka 1979, 1984, 1986 na 1991.
Alikabidhiwa jukumu la kuwa balozi wa nchi yake nchini
Uturuki tangu mwaka 2013. Ameacha mjane na mtoto mmoja wa pekee.
Siku ya leo amepigwa risasi wakati akihudhuria maonesho
ya sanaa za Kirusi mjini Ankara, tukio lililokatisha maisha yake.
0 comments:
Post a Comment