Kwa uchache watu 33 wamepoteza maisha na wengine 48
kujeruhiwa katika shambulizi la bomu lililotegwa kwenye gari katika kitongoji chenye
shughuli nyingi cha Sadr mjini Baghdad nchini Iraq, duru za kipolisi na
hospitali zimesema.
Mpaka sasa hakuna kundi lililodai kuhusika lakini kundi
la Daesh (Dola la Kiislamu katika Iraq na Sham) mara kwa mara limekuwa
likiyalenga maeneo ya raia katika mji huyo wenye ulinzi mkali.
Mapema siku ya Jumamosi mashambulizi matatu ya bomu
yaliwaua watu 29 katika mji huo. Shambulizi lingine la Jumapili liliwaua polisi
saba.
Vikosi vya serikali kwa sasa vinapambana kuliondoa kundi
la Daesh katika mji wa kaskazini wa Mosul, ambao ndio ngome kuu ya mwisho ya
kundi hilo katika nchi hiyo, lakini kumekuwa na upinzani mkali.
Tangu operesheni hiyo ilipoanza Oktoba 17, vikosi maalum
vimeichukua robo ya mji huo katika operesheni kubwa kabisa ya ardhini kutokea
nchini humo tangu Marekani ilipofanya uvamizi mwaka 2003 na kumuondosha kiongozi
wa zamani wa nchi hiyo, marehemu Saddam Hussein.
Waziri Mkuu Haider al-Abadi amesema kuwa mpaka Aprili
kundi hilo litaondoshwa kikamilifu katika maeneo yote ya nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment