Ndege moja ya mizigo ya Kituruki iliyokuwa ikijaribu
kutua katika uwanja mkuu wa ndege nchini Kyrgyzstan imeanguka katika kijiji
kimoja na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 32.
Kwa mujibu wa uongozi wa uwanja huo, ndege hiyo
iliyokuwa ikitoka Hong Kong kwenda Istanbul ilitakiwa kutua katika Uwanja wa Manas,
nje kidogo ya mji mkuu Bishkek.
Wafanyakazi wa kikosi cha uokozi wameopoa mwili wa
rubani na wanakijiji 15, wizara ya afya nchini humo imesema.
Chanzo hasa cha ajali hiyo ya ndege hiyo aina ya Boeing
747 inayomilikiwa na shirika la ndege la ACT, hakijajulikana.
0 comments:
Post a Comment