Rais wa Senegal amesema kuna uwezekano rais wa Gambia
kuondolewa kwa nguvu za kijeshi katika kiti cha urais baada ya kukataa kukubali
kushindwa katika uchaguzi.
Akizungumza Ijumaa, Macky Sall amesema chaguo la mwisho
la mgogoro wa kisiasa Gambia ni kutumia nguvu za majeshi ya kimataifa
kumlazimisha Yahya Jamme akubali kushindwa katika uchaguzi.
Sall amesema Senegal ina matumaini kuwa mazungumzo ya
kisiasa na onyo alilopewa Jammeh kuhusu hatima yake hasa kushtakiwa katika mahakama za kimataifa
ni jambo ambalo litamshawishi rais huyo wa Gambia abadilishe uamuzi wake wa
kukataa matokeo ya uchaguzi.
Tahadhari hiyo ya rais wa Senegal imekuja siku chache
baada ya viongozi kadhaa wa nchi za Afrika Magharibi kujaribu kumshawishi
Jammeh aondoke madakrani lakini jitihada hizo hazijazaa matunda.
Siku chache zilizopita, Jammeh aliwashangaza na kuwaacha
vinywa wazi Wagambia na duru za kisiasa barani Afrika alipoyakataa katakata
matokeo ya uchaguzi, kama alivyopongezwa na kila mtu alipojitokeza hadharani
siku ya tarehe Pili Desemba kumpongeza Adama Barrow, mgombea urais kwa tiketi
ya muungano wa vyama vya upinzani hata kabla hajatangazwa mshindi rasmi wa
kinyang'anyiro hicho.
Rais Jammeh aliyakataa matokeo ya uchaguzi wa rais kwa
madai ya kile alichokiita makosa yasiyokubalika yaliyofanywa na Tume ya Taifa
ya Uchaguzi ya Gambia na kutaka uitishwe uchaguzi mwingine mpya.
0 comments:
Post a Comment