Kwa uchache askari 13 wameuawa na wengine 48 kujeruhiwa
baada ya bomu lililotengwa kwenye gari kulipuka jirani na chuo kikuu cha Erciyes
katika Mkoa wa Kayseri katikati mwa Uturuki, taarifa ya jeshi la nchi hiyo
imesema ikiwa ni wiki moja baada ya shambulizi la mjini Istanbul lililoua watu
44.
Mlipuko huo ulitokea majira ya saa 2:45 asubuhi kwa
majira ya eneo hilo wakati basi lililokuwa limebeba raia na askari waliokuwa
wakitoka kazini lilipolipuliwa na bomu lililotengwa kwenye gari, jeshi
limesema.
Jumamosi iliyopita, milipuko pacha ya mabomu nje ya
uwanja wa soka katika mji wa Istanbul iliua kiasi cha watu 44 na kuwajeruhi
wengine zaidi ya 100.
Kundi la wanamgambo wa Kikurdi lijulikanalo kama Tai
waanaopigania uhuru wa Kurdistan au TAK, lilidai kuhusika na mashambulizi ya
Istanbul. Inaaminika kuwa TAK ni tawi la kundi la wapiganaji wa Kikurdi,
maarufu kama PKK.
Serikali ya Uturuki imekuwa ikipambana vikali na kundi
la PKK na makundi mengine ya Kikurdi, ambayo Ankara inayaona kama kitisho cha
usalama na imeyaweka katika orodha ya makundi ya kigaidi.
0 comments:
Post a Comment