Rais wa Gambia, Yahya Jammeh akimsikiliza mmoja wa wasaidizi wake mjini Banjul, wakati wa kufunga mkutano wa kampeni |
Kiongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika
Magharibi amesema kuwa viongozi wa nchi hizo watatuma askari kwenda Gambia iwapo
rais wa nchi hiyo aliyeshindwa uchaguzi hatoachia madaraka mwezi ujao.
Marcel de Souza amewaambia waandishi wa habari kuwa
Jumuiya hiyo imeichagua Senegal kuongoza kikosi cha kijeshi iwapo Yahya Jammeh
hatokabidhi madaraka Januari 19 ambayo ndio mwisho wa muhula wake kikatiba.
Akizungumza na wanahabari mjini Bamako nchini Mali, De
Souza amesema kuwa bado Jumuiya hiyo inaendelea kutumia njia za kidiplomasia
kumshawishi Jammeh akubali kuachia ngazi.
Jammeh aliingia madarakani miaka 22 iliyopita na amekuwa
akituhumiwa kuwafunga na kuwatesa wapinzani wake.
Aliwashangaza Wagambia na dunia kwa ujumla alipokubali
kushindwa uchaguzi lakini baadaye akabadili kauli.
0 comments:
Post a Comment