Balozi wa Ugiriki nchini Brazil Kyriakos Amiridis (katikati) |
Afisa mmoja wa polisi katika mji wa Rio de Janeiro
nchini Brazil amekiri kumuua balozi wa Ugiriki nchini humo, yumkini kwa
maelekezo ya mke wa balozi huyo ambaye yasemekana alikuwa na uhusiano naye wa
kimapenzi, duru za polisi zimesema.
Kituo cha televisheni cha Global cha nchini humo
kimenukuu duru hizo zikisema kuwa mapema Ijumaa mchana, afisa huyo aitwaye
Sergio Moreira mwenye umri wa miaka 29, alikiri kumuua balozi Kyriakos Amiridis siku ya tarehe
26 Desemba.
Mke wa balozi huyo,
aitwaye Francoise, ambaye ni raia wa Brazil, anashikiliwa na jeshi la polisi.
Wapelelezi wa jeshi la
polisi wanasema kuwa waliamini kuwa Francoise na Moreira walikuwa wamepanga
mauaji hayo, kituo hicho cha TV kilisema.
Jioni ya Alhamisi polisi
waliukuta mwili ulioungua ndani ya gari iliyokuwa imekodishwa na Amiridis.
Polisi mjini humo
wamekataa kutoa kauli yoyote kuhusu uchunguzi wao. Ubalozi wa Ugeriki mjini
Brasilia, nao ulikataa kutoa kauli.
Mjini Athens, msemaji wa
Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Ugeriki, Stratos Efthymiou, alisema kuwa
serikali haina kauli yoyote kwa sasa.
Mapema Alhamisi, polisi
walithibitisha kuwa balozi huyo alikuwa ametoweka tangu Jumatatu usiku ambapo
mara ya mwisho alionekana akiondoka nyumbani kwa familia ya mkewe katika
kitongoji kimoja chenye ghasia nyingi mjini Rio.
Taarifa za kupotea kwake
ziliripotiwa na mkewe siku ya Jumatano.
0 comments:
Post a Comment